Wanaume wengi hawasafishi mikono baada ya kujisaidia

Wimsha

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
518
503
Amani iwe kwenu wana JF,

Leo nimeona nizungumzie katafiti uchwara kadogo nilikokafanya juu ya usafi binafsi hasa wa wanaume. Wanaume wengi wakitoka kujisadia haja ndogo huwa hawanawi mikono. Kwa maneno mengine ukipeana mkono na mwanaume kuna uwezekano umeligusa dude lake kidigitali. Hali hii inachagiwa sana na kukosekana na maji safi/sabuni hasa sehemu za watu wengi baa, kumbi za starehe n.k . ingawa kuna baadhi ya wanaume wamekiri kuwa hata nyumbani huwa hawanawi mikono.

Wewe unanawa mkono baada ya kujisaidia haja ndogo?
 
Ni Vyema Ungefanya uchunguzi wa Kujua kwanza Athari za Hao Wasio nawa na Ukaja Na Majibu kwamba Kati ya Wanaume 100 waliotoka haja ndogo niliowapima nimewakuta Wanamaambukizi kwenye mikono

Ila Siyo Kuja Na Hisia Zako za Kinyaa Na Kusema Ni Utafiti...
 
Wengi watakuzodoa ila hilo ni swali fikirishi aiseee. Wafikirie tu na kwa wale wasio nawa mikono yao wawe wananawa sababu ni wachache wenye kufanya hiyo kitu.

Hata kama wakisema hawashiki mkojo ila ipo haja ya kunawa kila baada ya kufanya hiyo kitu.
 
Ni Vyema Ungefanya uchunguzi wa Kujua kwanza Athari za Hao Wasio nawa na Ukaja Na Majibu kwamba Kati ya Wanaume 100 waliotoka haja ndogo niliowapima nimewakuta Wanamaambukizi kwenye mikono

Ila Siyo Kuja Na Hisia Zako za Kinyaa Na Kusema Ni Utafiti...

Ndio maana nimeuita utafiti uchwara:)
 
Amani iwe kwenu wana JF,

Leo nimeona nizungumzie katafiti uchwara kadogo nilikokafanya juu ya usafi binafsi hasa wa wanaume. Wanaume wengi wakitoka kujisadia haja ndogo huwa hawanawi mikono. Kwa maneno mengine ukipeana mkono na mwanaume kuna uwezekano umeligusa dude lake kidigitali. Hali hii inachagiwa sana na kukosekana na maji safi/sabuni hasa sehemu za watu wengi baa, kumbi za starehe n.k . ingawa kuna baadhi ya wanaume wamekiri kuwa hata nyumbani huwa hawanawi mikono.

Wewe unanawa mkono baada ya kujisaidia haja ndogo?
Ukweli ulioje! Hasa kwa nchi zetu za Afrika. Ukiwa baa yoyote hapa Tanzania wanaume wengi wanaokwenda kijisaidia haja ndogo hawanawi mikono, hata kama kuna bomba na maji safi. Lakini kinachokera zaidi ni kuwa bar na hotel nyingi ukiingia vyooni unakutana na gudulia moja kubwa lenye maji na kopo kwa pembeni! Sasa kunawia maji na vifaa vya kuchangia yya aina hii wengine wanaona ni bora wasepe bila kunawa!
 
Unashangaza kweli...

Sasa ile si ni ngozi ka ya usoni tu.
 
mbona uku mikoani hatunawi na wala hao bacteria wenu wa mjini hatuwapati sijui sifurococas na wenzake, in short amini ukifanyacho na usitie hofu hutopata gonjwa lolote
 
kushika ududu ni sawa nakushika ngozi ya mkono so nothing gonna happen, labda kama mkono wako utagusa vitone vya mkojo au una ugonjwa wa ngozi.
 
Back
Top Bottom