mtaa umetulea
JF-Expert Member
- Nov 17, 2020
- 1,719
- 2,165
Hahaha kula mzigo kwa shida
Kuna jamaa bonge mwenzangu alianza mazoezi, akajinyima kula, akanunua madawa ya C9, akawa analipia Gym elfu 60 kwa mwezi na kuhudhuria kila siku.
Baada ya mwaka kilo ziliongezeka kutoka 105 hadi 119.
Kuna miili mingine ni ya kurithi. Kama imo imo tu.
"hatutumiki kwenye matangazo ya kuonyesha upendo zaidi ya kuwekwa kwenye KOPO LA MAZIWA"
Pole sana mkuu
Natamani kitambi aseee, niwe nafutia kioo cha infinix yangu.
Asante kwa ushauri Muuza simu used ama kweli wazijua simu na namna ya kuzitunza.Kitambi cha kufutia infinix hakikisha uwe unafakamia viporo kila kukicha Asubuhi!ila kama cha kufutia IPhone latest inabidi utumie akili nyingi sana
pia mnakula sana, yani bonge akikutangullia kwenye bufee umekwisha.wanaume wanene tunanyanyasika sana,ukiwa unakula kitu kizuri anapita mwembamba utasikia,"UNAHARIBU MWILI WEWE".Nikipata dada mzuri hata kabla ya kufurahi naye utasikia hee"WE MNENE KWELI PUNGUZA TUMBO,bila hata ya kujali tumbo linabonyea.Mara nyingi tukiwa kwenye makundi tunashindwa kula kwa kujiachia kuhofia watu mwisho wa siku tunabeba sana take away,kwenye jogging club nyimbo zote za fedheha zinatuhusu,kwenye post card hatujawahi kuwekwa,na hatutumiki kwenye matangazo ya kuonyesha upendo zaidi ya kuwekwa kwenye KOPO LA MAZIWA,Sisi wenyewe tumejikubali kwa kukubali kupata shida kuinama,kufunga kamba za viatu,kuhemea juu juu,kushindwa kukimbia kula mzigo kwa shida LAKINI KIUKWELI SISI WANAUME WANENE NI ISHARA YA UVUMILIVU KWANI UWEZO WA KUZULULA NA MATUMBO YETU NI USHUJAA TOSHA,Mwisho wa siku wanene sisi tuna vimbinu vya kupata pesa.WANAUME WANENE HOYEEEEE