Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,405
Uko kwenye ndoa mwaka wa tisa huu. Mke wako ulimuoa alipomaliza form four na kubahatika kupata watoto wawili. Kwa msisitizo wako mke amekwenda chuo na kumwacha mtoto mdogo akiwa na miaka miwili.
Kwa msaada wa mama mkwe, mmepata kabinti kamemaliza darasa la saba anatafuta kazi. Kwakuwa una shida ya mlezi wa watoto umeamua kumchukua na umekubali kuwa shughuli nyingi unafanya mwenyewe ukitoka kazini au weekends, yeye alee watoto tu.
Mwaka wa saba huu binti anapendeza . Mkeo ni mwajiriwa sasa baada ya kupata diploma. Binti huyu anakuangalia kama baba yake kwani umemlea .
Usivyo na haya unamtongoza kwa ahadi ya kuwajengea wazazi wake nyumba. Akifikiria hali ya kwao anakubali mnaanza mchezo. Mara binti ana mimba.
Mke wako anataka kumrudisha kwao , kidume unafanya jitihada zote kumpangishia chumba mjini. Anazaliwa mtoto wa kiume. Kwakuwa una two girls njia kuu, unachanganyikiwa na nyumbani unapotea siku mbili hujali kupishana vikumbo chooni kwenye shared house.
Wanaume kweli mnayaweza.