Wanaume wanaopenda lift....

Wanaume wanaopenda lift....

Tungekuwa na Moyo wa upendo kwa kila mtu ingependeza! Usione kutoa lift ni tatizo ! Mola ndo anapanga yote anamnyima yeye anakupa wewe ili tutegemeane!Hivi angeweka usawa kwa watu wote ingekuwaje? Kila Mtu amiliki hummer, Fedha, Mali, n.k nani angemtumikia mwenzie!?
Kila mwenye gari asubuhi angebeda watu japo 4 au kulingana na uwezo wa gari lakie tatizo la usafiri lisingekuwepo!
Mpende jirani yako kama Nafsi yako!
Kuna mama mmoja aliombwa lift akamyima yule aliyemuomba! jamaa akaamua kutembea kwa mguu kufika mbele akamkuta mama anaomba msaada gari lake limekwama kwenye tope! Alichokifanya jamaa alimsaidia mama kutoa gari lile kwenye tope kisha akaendelea kutembea kwa mguu

Nimeipenda hii
 
Haaahaaaaa, watu wanataka wapakie mademu mbele ya safari halafu nyie mnaleta viwingu kwa tiketi ya jirani! Kudadeki babaake... Halafu eti 'wabongo tunapendana' wapi bana. Hivi na wanawake wenye mikoko huko bongo huwa wanatoa lifti kweli?
 
Mtoa uzi kusema kweli sikuungi mkono, hivi kama gari ni la siti 5 na uko peke yako au na my wife wako tu ukipakia na majirani 2 (Ambao ndio watakukimbilia siku ukipata shida usiku) unakuwa umeharibu au kupunguza nini jamani, mafuta si ni yale yale mkuu? Kama ni praivesi na wife si mnalala chumba kimoja jamani na kama siku hutaki kumpakia mtu anakupigia simu si unamwambia tu kuwa nina mizunguko kidogo leo, Nilidhani labda ungeona ufahari kuwa unasaidia watu kwa roho nyeupe kumbe unasaidia huku unaumia!

Kusaidia watu ni vizuri mkuu, inaongeza sana amani moyoni kwako na maishani kwako, huna haja kumsimanga mtu ambae kabisa unajua msaada wako ni muhimu kwake na shukrani yake ni thawabu kwako Boss!

Ngoja siku akina Lord Eyez wamwibukie na wakombe kkagari kake akipiga mayowe usiku sijui kama majirani watatoka, tujifunze kuishi vizuri na majirani zetu wewe Mungu kakupa mafanikio unamiliki mkoko mwenzio hana lakini kwa namna ya pekee Mungu kamjalia kitu kingine yawezekana wewe huna ishini vizuri na watu gari lisikufanye ukakosa utu na kuwadharau wasio kuwa nalo.
 
Kama huna usafiri binafsi na bora kusubiri usafiri wa umma, lift ikitokea iwe ni bahati nzuri. Kuhangaika kuombaomba ni kunajidhalilisha bila sababu za msingi.
 
Tumejua una gari wiyelele mashauzi yote haya ukute una kiusafiri cha Vitz au Duet au Swift!!! Kuna kijana mwenzetu nae alikopa bank banaaa akawa anatufungia vioo kituoni kama hatuoni! Sie hatuna iyana tunapanda dala twaenda!!!!!!

Mungu si Lara 1, hamad siku kimkweche chake kikazima mbele kidogo ya kituo baada ya kutupita! Akarudi kutusalimu na miguu na kutuomba tumuangalizie gari aende ATM hadi fundi aje! Kila mtu akageuza shingo pembeni kama hatumjui vileee! Hamna aliejibu, dala ikaja hao tukaishia zetu! Alijambajeee sasa, kwenda ATM kurudi wamekwapua power window, taaa, site mirror, taa acha kabisaa! Chezea Kino usiku!
mwenyewe nahisi mleta mada anataka tujue ana usafiri
 
Hahahahaahaaaaaaaaaaaaa! wera weraaaaaaaaaaaaaa! Wilyelele Hongeraaaaaaaaa! Duh! sikufahamu kama umenunua Gari, Basi utanikuta namim pale kituoni kesho, na sitachangia mafuta. Khaaaaaaaaaa! kama kawaiada yako.

Ni mwaka wa sita tangu niwe na gari na wala sio mpya. Ila naona hii tabia inakera sana. Kuna jamaa kila siku mi na jirani yangu tulikuwa tunampa lift yeye na mke wake na alikuwa mpole sana. Siku aliponunua VITZ yake, aliacha hata kutusalimia!
 
Kwanini unashindwa kuwatoza nauli?

Watanitangaza mtaa mzima...ila hawa wanaonisumbua sio majirani zangu. Ni washikaji tu ambao wanavizia barabarani, ukimpa lift siku moja anazoea gari na kila ukipita anakupiga mkono. Angalabu kama ningekuwa nimesoma nao lahasha! Unampa mtu lift kila wakati anakuambia punguza sauti ya redio anaongea na simu kila wakati! Mwingine mara oho sijazoea AC nataka fungua vioo! Sasa inakuwa kero wapande daladala tu ambazo kila wakati vioo viko wazi
 
Wiyelele kama wanaokusumbua ni jamaa zako- waambie ukweli tu.


Binafsi napenda sana kutoa lift hasa asubuhi , ni jambo jema kushiriki ulichonancho na wengine. Ila iwe unplanned, kama unatoka na unaona jirani wanaelekea kituoni si vibaya ukiwapa tafu kwenda nao job au town.


But the other side of the coin ni binadamu tuna tabia ya kujisahau sana kama incidents zifuatazo:

1)Kuna jamaa nilikuwa nampa lifti nikiwa naenda job, basi akawa amezoea ile mida- baada ya siku kadhaa kila nikitoka getini namkuta hapo nje ya geti ananisubiri nitoke. Basi baada ya siku kadhaa tena , akawa anagonga kabisa geti kama saa kumi na mbili , ili aingie asubirie kwa ndani. Ikatokea siku moja siendi kazini basi kama kawaida kagonga na kwa kuwa ni jirani dada wa kazi kamfungulia , akakaa barazani - muda umepita mi nimejilalia zangu. Mara nasikia mtoto anagonga chumbani, ooh kuna mgeni, kutoka ndio yule jamaa wa lifti. Basi nikamwambia leo siendi job, duh jamaa bila aibu akaniuliza "mbona hujanipigia simu kuwa huendi?". Basi nikamwambia mimi huwa sina ratiba maalumu wewe uwe unaenda kituoni nikikukuta sawa, else consider am not around.

2) Niliwahi kuwapa watu fulani lifti mara mbili tatu: kila wakipanda mi nina CD yangu ya old music napenda kusikiliza, basi wakiingia tu- wanasema aaah weka BBC bwana tusikie habari. Sasa wewe ulikuwa unatembea tena kimya kimya, kupanda tu kamkweche kangu unadai BBC?

3) Kuna baadhi ya jamaa fulani ikifika mda ya kutoka kazini, text message na simu ooh unatoka sangapi. Na mi bila hiyana nasema. Sasa ikawa wakipanda wanaanza ooh naomba tusimame pale kontena ninunue LUKU , ooh kuna mtu ana bahasha yangu kituoni simama kidogo, mwingine anakuja na rafiki yake. Sasa kweli hapa utasema ustaarabu upo?

4) Siku moja niliwaambia watu walioniomba lifti jioni kuwa leo napitia maduka fulani ya ujenzi: bila aibu wakasema aah haina shida kwani utachukua muda. Basi kufika lile duka wakawa hawana stock inabidi niende kwenye godown yake ingine. Ikawa embarassment maana ilibidi niwaambie safari imebadilika na siendi home.

5) Huyu mmoja namsamehe maana hata mimi yanaweza nikuta, nimempa lifti na mtoto akawa amesahau kadi ya hospital, so akaomba turudi all the way apick kadi. Kurudi kafoleni kakawa kameanza, baada ya kama dakika 20 hivi mtoto wa around 3 yrs akadai kujisaidia basi ikabidi tupaki ashuke na ajisaidie.


Wito wangu mimi ni: kama jamii kusaidiana ni muhimu. Si vyema kwa mwenye gari kuwa mchoyo. We werent born with anything. Kuna vitu vidogo unaweza mezea (no one is perfect). Ila na kwa wapewa lift , chonde chonde usizoee kiasi cha kuwa dikteta sana. Kwenye kila jambo kuwe na mipaka.
 
Hii maneno ilinifanya nijisikie hovyo sana! Sisemi kitu hapa nakula chabo tu michengo inavyomwagwa, mweeeeeee!
 
mie nlikuwa natoa lift walikuwa wanajua muda nnaotoka kwahio na wenyewe ndio wanatoka na kunisubiri njiani ukiwapita nooma halafu mlango wanabamiza. gari ilikuwa inajaa watu 4 nyuma kama fastjet kulaleki. nilipohama mtaa nikipita karibu na kituoni najifanya naongea na simu huyo napaisha ngoma sijui nini kilikuwa kinatokea.
 
mie nlikuwa natoa lift walikuwa wanajua muda nnaotoka kwahio na wenyewe ndio wanatoka na kunisubiri njiani ukiwapita nooma halafu mlango wanabamiza. gari ilikuwa inajaa watu 4 nyuma kama fastjet kulaleki. nilipohama mtaa nikipita karibu na kituoni najifanya naongea na simu huyo napaisha ngoma sijui nini kilikuwa kinatokea.

hahahaha
we
ni
nomaa.
 
mie nlikuwa natoa lift walikuwa wanajua muda nnaotoka kwahio na wenyewe ndio wanatoka na kunisubiri njiani ukiwapita nooma halafu mlango wanabamiza. gari ilikuwa inajaa watu 4 nyuma kama fastjet kulaleki. nilipohama mtaa nikipita karibu na kituoni najifanya naongea na simu huyo napaisha ngoma sijui nini kilikuwa kinatokea.


nachukia sana tabia ya kubamiza milango! Mwingine anaanza kubadilisha stesheni ya redio bila aibu. Na kuna wale ambao wakipanda watakupa masharthp ya kuwasha na kuzima ac
 
Back
Top Bottom