Wanaume wanaopenda lift....

Wanaume wanaopenda lift....

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Posts
1,071
Reaction score
348
Napata shida sana na hili. Wote tunafahamu kwamba jiji la Salidalama lina tatizo la usafiri na pengine kumsaidia mtu ni kitu cha kawaida kama anakwenda kazini. Lakini cha ajabu, kuna baadhi ya wanaume ambao wanafanya kazi. Kila siku unamkuta mtu amesimama mbali na kituo cha daladala utafikiri anasubiri gari la ofsini kwao kumbe sio. Kila akipita mtu unakuta kazi ni kuchungulia kwenye vioo vya gari na kupiga mkono kama trafik. Ukiwa job anapiga unatoka saa ngapi ili apande tena wakati wa kurudi home.

Jamani kwa nini wanaume tunajifedhehesha hivi? Mtu anakupa lift maramoja na pale ambapo kweli kuna shida ya usafiri na wewe, jaribu kukaa hapo kwenye kituo cha mabasi na wenzako. Wanaume tusipende sana kudandia lift maana ni fedheha. Mambo haya yalikuwa kwa wanawake zamani lakini siku hizi yamehamia kwa wanaume!

Najua wengi wataponda lakini ukweli ndo huo! Mi na mke wangu hatukuwahi kudandia lift ya mtu, tulikwa sisi na daladala kila siku! Hata kama gari imeleta tatizo tulikuwa tunawahi kupanda daladala. Iweje wasio na magari wapende sana lift utafikiri shida hawana?
 
Duh! hii hali ilifanya nikaacha kuendesha gari maana nilikaribia kuvunjiwa heshima na mke wa mtu kisa, nampa lift mumewe lol!
 
neno hilo......

leo acha nikuunge mkono...

uko na my waifu wako mnashindwa hata kuja**a..inahuuu.....

inaeleweka kumpa lifti myu asubuhi lakini huyo hadi jioni anakupigia kukuuliza lifti amepitiliza, hajui mjini kila mtu ana mipango yake? huo ndo muda wa kwenda kwenye mishe mishe binafsi...aache...

anyway mkiwa mnatumia tz 11 kama sie hutosumbuka na lifti, maana lifti ni miguu yake tu...

Asprin uko wapi? nimekumiss
 
Last edited by a moderator:
khaaaaaaaaa yaani unaacha kuendesha gari lako ulonunua kwa pesa yako kwa sababu ya mtu? si unawapa tu za uso na unaacha kuwapa lifti?

Duh! hii hali ilifanya nikaacha kuendesha gari maana nilikaribia kuvunjiwa heshima na mke wa mtu kisa, nampa lift mumewe lol!
 
Ila mkumbuke sio kila mtu ana uwezo wa kununua gari, na kila mtu akinunua gari nani atapanda daladala???kama unaweza mpe mtu lift kama huwezi basi tuu. Sio lazima kumpa mtu lift na ukishampa mtu lift sio vizuri kumsema tenaa. Jamani mungu ni mmoja tu anayetuma hayo magari........
 
Sawa hilo ni kweli lakini sio kila siku ndo gari la mtu ulifanye lako na yeye awe dereva wako!
 
Kuna leo na kesho mkuu..kesho nawe waweza kukosa hata aliyekupa wewe naye ana makusudi yake na ukimpa mtu msaada hautakiwi kuhesabu.
 
sioni tatizo kama ni majirani/rafiki na mnafanya kazi sehemu moja na timetable zinaendana. although sipendi kutoa random lift kutokana na usalama
 
Tumejua una gari wiyelele mashauzi yote haya ukute una kiusafiri cha Vitz au Duet au Swift!!! Kuna kijana mwenzetu nae alikopa bank banaaa akawa anatufungia vioo kituoni kama hatuoni! Sie hatuna iyana tunapanda dala twaenda!!!!!!

Mungu si Lara 1, hamad siku kimkweche chake kikazima mbele kidogo ya kituo baada ya kutupita! Akarudi kutusalimu na miguu na kutuomba tumuangalizie gari aende ATM hadi fundi aje! Kila mtu akageuza shingo pembeni kama hatumjui vileee! Hamna aliejibu, dala ikaja hao tukaishia zetu! Alijambajeee sasa, kwenda ATM kurudi wamekwapua power window, taaa, site mirror, taa acha kabisaa! Chezea Kino usiku!
 
Hata VITZ au Duet ni gari na haziitwi boda boda. Sisemi ni vibaya kumpa lift mtu ndo maana nawapa lift. Hawo ninaowapa si wafanyakazi wenzangu wala majirani. Ila mtu ambae unazoeana nae kidogo na ukamsaidia siku moja basi yeye anakariri haka ka "VITZ" na kukavizia kila siku. Mbona mi na mke wangu tulisota sana bila kujiaibisha kwa lift za watu? Hata siku hizi kuna wakati tunajipandia daladala wakati majirani wana magari... Kwanini mtu uvizie lift ya mtu kila wakati na akiwa job akose raha ya kupokea simu yako kumsumbua ni wakati gani anatoka ili udandie tena?
 
Basi msaidie mwenzio.. Kama vipi mwambie achangie mafuta.. Nafahamu kuna watu huwa wanachanga mafuta

Hili la kuchangia mafuta kuna siku walipanda watu watatu, wakati nanunua mafuta, mmoja alitoa elf kumi. Baada ya wiki nikasikia eti wanachangia mafuta ndo maana gari liko barabarani kila siku. Nilichokifanya ni kutochukua hela ya mtu ata akitoa nakataa kabisa.
 
Back
Top Bottom