Wanaume walioko kwenye ndoa wana raha sana

HARUFU
Waambie walalamishi RAHA za ndoa.
Mke sio jiko wala sio mtoto wa kazi.Mke NI muungano wa wapendanao.Uzuri wake NI kukaa mbali Na familia zenu maana familia zina leta maneno mwisho FITNA inaingia kati yenu.
Nimeoa muda mrefu nampenda Mke Wangu sanaaaaa tu. Tunakwenda karibu kila sehemu pamoja ila kuna wakati anataka kuwa Na rafiki zake wa kike Na mimi nakwenda kijiweni.
Simu zetu hazina ufunguo(password) tunaishi Kwa Amani Na saa zote kapendeza
Mna mda gani Mkuu
 
Huyo atakuwa na less than 10 years katika ndoa huyo. Experence ya ndoa inaanza ukiishi katika ndoa angalau miaka 10, chini ya hapo bado mnatafuta fomula ya kuishi wote

Mkuu fomula NI kupendana kikweli sio kimaslahii.
 
Nampenda saaaana Mke wangu, kitu cha Tanga Mbondei halisi, yeye lake jiko,Nazi, Usafi wake na wangu, hana Makuu. Amefundwa na anaifahamu mipaka yake kwa mumewe. Siwezi kuacha simu hapo aanze kuipekua pekua au nimerudi kwa kuchelewa kidogo eti anune. Hahahaha kwa kweli Nina mpango wa kwenda kuongeza mahari naona kama Value ni kubwa kuliko nilichotoa. Ibada ikifika utakuta umeandaliwa kila kitu omba sasa ifike weekend Dah, Mara Juice, Mara supu Mara karanga utafune na asali kando ya kisosi. Dah
 
Jaribu nawe kuivua na kuiweka kabatini kisha msikilizie atasema? Au km haivai lkn still upendo, aman, furaha ipo na hujawah ona cheating zozote its fine
Hajali mkuu anakwambia pete sio kipimo cha upendo,so nivae sawa nisivae sawa,yeye kama sikutia Hinna mda mrefu ndio ataongea lakini sio pete lol..
 
Asante sisame.Ndoa zote zina mapungufu yake.Muhimu MARUFUKU kuishi Na ndugu wa upande wowote:Maana ndugu wa upande Wangu wanakuwa Na wivu Na mke wangu wa upande wa mke wanaona kila kitu NI chao.
Ukisema utaambiwa unawasimanga NI shida tupu.Mkiishi wawili pamoja Na watoto hakuna sintonfahamu.Tukitaka kwenda kwenye sherehe tunawapeleka Kwa bibi yao maana hatuna mtu wa kazi NI sisi tu.
Mmh wachoyo sana nyie
 
Mungu ni mkubwa,sisi wanaume tofauti ya kuwa single na kuwa kwenye ndoa ni ndogo sana!!
 
  • Thanks
Reactions: irk
Jioni ya Leo nikapokea simu ya bro, Dogo nakuja home kukuchukua nikale nawe bata za mwisho mwisho karibuni sikupati tena.

Leo nikasema wacha nikaoshe macho kabla sijaingia kifungoni, chezea maisha ya kuomba ruhusa. Tangu nipate tumbo nimekuwa mvivu nikasema sio mbaya wacha niende hivyo hivyo.

Sehemu zote tulizopita sijakutana/kuona Wanawake wenye Pete za Ndoa zaidi ni Wanaume wenye Pete za Ndoa na Wanawake wasio na Pete ama wako peke yao.

Nimebaki na maswali kibao yasiyo na majibu na mawazo juu, inamaana wakwangu naye atakuwa kama hawa na alivyo Mlevi yule bwana ntaweza kweli???
Wake zao wameshindwa kuongozana nao ama wamewakataza???
Au ndiyo ukiolewa wewe yako Nyumba???

Wanaume mnaraha sana maamuzi mikononi mwenu bila kujali umeoa ama una familia, wakati wowote unafanya unachojisikia bila kupangiwa na Mtu.
Kumuacha mwanamke nyumbani si wivu ni moja ya furaha na faraja aweze kupunzka na kukupokea vizur pind urudipo kwenye mishe
 
Nampenda saaaana Mke wangu, kitu cha Tanga Mbondei halisi, yeye lake jiko,Nazi, Usafi wake na wangu, hana Makuu. Amefundwa na anaifahamu mipaka yake kwa mumewe. Siwezi kuacha simu hapo aanze kuipekua pekua au nimerudi kwa kuchelewa kidogo eti anune. Hahahaha kwa kweli Nina mpango wa kwenda kuongeza mahari naona kama Value ni kubwa kuliko nilichotoa. Ibada ikifika utakuta umeandaliwa kila kitu omba sasa ifike weekend Dah, Mara Juice, Mara supu Mara karanga utafune na asali kando ya kisosi. Dah
Shukuru Mungu kwa kupata mke bora kiongozi.
 
Sehemu zote tulizopita sijakutana/kuona Wanawake wenye Pete za Ndoa zaidi ni Wanaume wenye Pete za Ndoa na Wanawake wasio na Pete ama wako peke yao.

Population census duniani inaonesha wanawake ni wengi kuliko wanaume.
 
Tatizo ukitoka na mke hakawii kuaharibu bajeti akipita muuza viatu kamuita,muuza vyomba anakumbuka nyumban vitu hani hamna atanunua hata chujio nae kamuita,akipita muuza nguo kamuita si,anajua yupo na ATM lakin ukitoka mwemyewe au reserve hakuna shida bajet inaenda vile ilivyopangwa.!
 
Nampenda saaaana Mke wangu, kitu cha Tanga Mbondei halisi, yeye lake jiko,Nazi, Usafi wake na wangu, hana Makuu. Amefundwa na anaifahamu mipaka yake kwa mumewe. Siwezi kuacha simu hapo aanze kuipekua pekua au nimerudi kwa kuchelewa kidogo eti anune. Hahahaha kwa kweli Nina mpango wa kwenda kuongeza mahari naona kama Value ni kubwa kuliko nilichotoa. Ibada ikifika utakuta umeandaliwa kila kitu omba sasa ifike weekend Dah, Mara Juice, Mara supu Mara karanga utafune na asali kando ya kisosi. Dah

Mkuu Eli nakuona umebwebwa Hongera sana
725b36d4f7992c06e1dc09ca14600749.jpg
 
Back
Top Bottom