Wanaume walioko kwenye ndoa wana raha sana

angelita

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
3,015
2,000
Jioni ya Leo nikapokea simu ya bro, Dogo nakuja home kukuchukua nikale nawe bata za mwisho mwisho karibuni sikupati tena.

Leo nikasema wacha nikaoshe macho kabla sijaingia kifungoni, chezea maisha ya kuomba ruhusa. Tangu nipate tumbo nimekuwa mvivu nikasema sio mbaya wacha niende hivyo hivyo.

Sehemu zote tulizopita sijakutana/kuona Wanawake wenye Pete za Ndoa zaidi ni Wanaume wenye Pete za Ndoa na Wanawake wasio na Pete ama wako peke yao.

Nimebaki na maswali kibao yasiyo na majibu na mawazo juu, inamaana wakwangu naye atakuwa kama hawa na alivyo Mlevi yule bwana ntaweza kweli???
Wake zao wameshindwa kuongozana nao ama wamewakataza???
Au ndiyo ukiolewa wewe yako Nyumba???

Wanaume mnaraha sana maamuzi mikononi mwenu bila kujali umeoa ama una familia, wakati wowote unafanya unachojisikia bila kupangiwa na Mtu.
 
HARUFU

Platinum Member
Jan 21, 2014
28,284
2,000
Nashindwa kumuelewa Mwanamme ambae hapendi kuongozana na Mkewe.

Sasa kama hajiamini na Mkewe, labda tuseme machoni mwa watu.

Sasa alimuolea nini?

Raha ya Ndoa ni pamoja na kuwa karibu na Mkeo mara kwa mara, na Watoto wenu.

Inapendeza sana na inajenga Upendo.

Onesha upendo kwa Mkeo
 
mgogoone

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
2,913

Waambie walalamishi RAHA za ndoa.
Mke sio jiko wala sio mtoto wa kazi.Mke NI muungano wa wapendanao.Uzuri wake NI kukaa mbali Na familia zenu maana familia zina leta maneno mwisho FITNA inaingia kati yenu.
Nimeoa muda mrefu nampenda Mke Wangu sanaaaaa tu. Tunakwenda karibu kila sehemu pamoja ila kuna wakati anataka kuwa Na rafiki zake wa kike Na mimi nakwenda kijiweni.
Simu zetu hazina ufunguo(password) tunaishi Kwa Amani Na saa zote kapendeza
 
JT2014

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
1,865
2,000
Kawaambie wanawake wenzio
wakiambiwa kutoka waache kuweka masharti
bali waone ni fursa muhimu,wakiweka masharti
huko barabarani kuna wasio na masharti.

Afu hata hao wenye pete
zinaweza kuwa za ndoa tofauti
wewe ukadhani ni za ndoa moja
na wasio napete,huenda zilishawabana
wakaachana nazo lakini ni wanandoa.
 
sisame

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
364
500
HARUFU
Waambie walalamishi RAHA za ndoa.
Mke sio jiko wala sio mtoto wa kazi.Mke NI muungano wa wapendanao.Uzuri wake NI kukaa mbali Na familia zenu maana familia zina leta maneno mwisho FITNA inaingia kati yenu.
Nimeoa muda mrefu nampenda Mke Wangu sanaaaaa tu. Tunakwenda karibu kila sehemu pamoja ila kuna wakati anataka kuwa Na rafiki zake wa kike Na mimi nakwenda kijiweni.
Simu zetu hazina ufunguo(password) tunaishi Kwa Amani Na saa zote kapendeza
Hongera mkuu, hii ndio maana kamili ya ndoa!
 
mashahu

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
517
250
Nashindwa kumuelewa Mwanamme ambae hapendi kuongozana na Mkewe.

Sasa kama hajiamini na Mkewe, labda tuseme machoni mwa watu.

Sasa alimuolea nini?

Raha ya Ndoa ni pamoja na kuwa karibu na Mkeo mara kwa mara, na Watoto wenu.

Inapendeza sana na inajenga Upendo.

Onesha upendo kwa Mkeo
wanawake wengine visirani, wakitoka na waume zao lazima mtarudi mmenuniana, ndo maana wanatoswa nyumbani.
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
16,964
2,000
Ndio ni nzuri ikiwa na Baraka za Mungu.

For sure, hiyo itakuwa ni NDOA vinginevyo ni maigizo....hasa kwa dunia yetu hii ya sasa.
 
Roger Sterling

JF-Expert Member
May 10, 2015
12,311
2,000
Sio lazima wanandoa watoke pamoja kila muda, kila mahali. Mnahitaji time-out kila baada ya muda. Pengine hata wake za hao jamaa walikuwa kwenye mitoko yao tofauti, kivyao.

Anyway, hongera kwa harusi na kijacho. Can tell the excitement.
 
tejay

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,255
2,000
Jioni ya Leo nikapokea simu ya bro, Dogo nakuja home kukuchukua nikale nawe bata za mwisho mwisho karibuni sikupati tena.

Leo nikasema wacha nikaoshe macho kabla sijaingia kifungoni, chezea maisha ya kuomba ruhusa. Tangu nipate tumbo nimekuwa mvivu nikasema sio mbaya wacha niende hivyo hivyo.

Sehemu zote tulizopita sijakutana/kuona Wanawake wenye Pete za Ndoa zaidi ni Wanaume wenye Pete za Ndoa na Wanawake wasio na Pete ama wako peke yao.

Nimebaki na maswali kibao yasiyo na majibu na mawazo juu, inamaana wakwangu naye atakuwa kama hawa na alivyo Mlevi yule bwana ntaweza kweli???
Wake zao wameshindwa kuongozana nao ama wamewakataza???
Au ndiyo ukiolewa wewe yako Nyumba???

Wanaume mnaraha sana maamuzi mikononi mwenu bila kujali umeoa ama una familia, wakati wowote unafanya unachojisikia bila kupangiwa na Mtu.
Kila kitu kina faida na hasara zake
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,757
2,000
Olewa sie tuvae nguo zetu tumenunua kwenye sale. Wewe ukianza shule ulikuwa unajua kuandika?Olewa kwanza mdogo wangu, halafu tutakupa mbinu za kufurahia ndoa. Yaani umenichekesha kweli hahaha.
 
NIMPENDENANI

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
6,131
2,000
Pete ya Ndoa ya mume wangu iko kwenye safebox miaka 16 sasa aliivaa kwenye sherehe tuu baada ya hapo inahama kutoka side A kwenda side B ya safebox,kama kuna kitu nimeshindwa kumlazimisha nikuvaa pete..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom