Ubishi wa ulazima mwanamke kuolewa au kutoolewa utaisha lini?

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,711
3,361
Kuna kundi la wanawake wanasema hakuna ulazima wa mwanamke kuolewa au kuishi na mwanamume maana saivi kila mtu anajiweza bila kujali ni wa jinsia gani na hata kama mwanamke ataolewa basi hakuna utofauti wowote na yule asiyeolewa.

Lakini kuna kundi la pili la wanawake linasema ni lazima mwanamke mkamilifu aolewe kwa kuwa mwanamme ni kiongozi aliyeumbwa kuongoza familia.

Kundi hili limeenda mbali zaidi kwa kudai kuwa wale wanawake wenzao wanaodai hawaoni umuhimu wa kuishi na mwanamme eti 'wanajishauwa tu' ila kiukweli hata wao wanatamani kuwa na wanaume ila ndoivo tena mipango imebuma!.

Wanadai kuwa wanawake hawa maarufu kama 'masingomaza' wakirudi vyumbani mwao huwa wanalia wenyewe kimyakimya na kujuta sana kwa maisha ya upweke ya bila kuwa na wenza.

Wakuu binafsi nahisi kuchanganyikiwa na hoja za makundi haya mawili kinzani kiasi sijui wapi wanasema ukweli.

Wewe unawaamini wepi kati ya makundi haya mawili?
 
Back
Top Bottom