Wanaume wa JF mnaweza kufanya hivi?

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,971
35,113
Habarini wanaJF.

Niende kwenye mada bila kuchelewesha muda, ni hivi kuna jirani yangu ambaye kabla ya kuolewa na mume aliye naye alikuwa tayari amezaa mtoto anayeitwa Mary na bwana mwingine.

Jana baba yake Mary akaja nyumbani kwa mzazi mwenzie kumuona mwanae.
Mume wa ndoa wa huyu mama alikuwepo home, pia mama Mary alikuwepo.
Mama Mary na mumewe wa ndoa walimpokea kwa bashaha Baba Mary.
Walikaa pamoja, yaani mume wa Mama Mary wa sasa ambaye wamefunga ndoa, Huyo mzazi mwenzie mama Mary ambaye ndie baba Mary halisi, Mary mwenyewe na Mama Mary walikuwa wanaongea na kucheka kwa furaha.

Baadaye mgeni wao (mzazi mwenzie mama Mary) aliaga na wote kwa pamoja akiwemo mume wa ndoa wa mama Mary walimsindikiza na kuagana kwa furaha.

Majirani wambeya wambeya tulikuwa tunachungulia tu na kufurahia amani iliyokuwa imetawala eneo lile na hasa kuona jinsi mume wa ndoa wa huyu mama alivyokuwa hana wivu, ni MNYAKYUSA na mama Mary ni Mzaramo, Baba Mary halisi ni Msukuma

Nawasilisha
 
Hakuna tatizo hapo, hiyo inaonesha ukomavu wa akili, upendo na heshima kwa wote. Lazima tukubali historia zilizopita za wapenzi/wana ndoa wenzetu. Sio kila jambo ni la kutilia mashaka ili mradi kila mmoja ana nia njema.

Ila sikuona sababu ya wewe kutaja makabila ya wahusika. Tukio unalolielezea halina uhusiano na makabila yao. Laweza kutoa kwa mtu wa kabila lolote au lisitokee.
 
hahahahaah, mbona umenifananisha na Mondray?!!!!!!!! hahahahah, ila nasikia hata kule umasaini, kama mlifanyiwa jando pamoja nikimaanisha mko rika moja, mwenzako anaweza kufika home kwako, akachoma mkuki hapo mlangoni halafu yeye akawa ana mkamua my wife wako! wewe ukija ukiona mkuki unapotezea hadi mwenzio amalize ndio unagonga hodi, hahahahahahahaha Daby, good morning
Nmeshindwa kusoma hapo juu tatizo unacharaza sana kama Dr. Adams faida.

Mondray si alikuwa anakuita Chikila

Nimeamka Salama tunashukuru kwa uhai
 
Habarini wanaJF.

Niende kwenye mada bila kuchelewesha muda, ni hivi kuna jirani yangu ambaye kabla ya kuolewa na mume aliye naye alikuwa tayari amezaa mtoto anayeitwa Mary na bwana mwingine.

Jana baba yake Mary akaja nyumbani kwa mzazi mwenzie kumuona mwanae.
Mume wa ndoa wa huyu mama alikuwepo home, pia mama Mary alikuwepo.
Mama Mary na mumewe wa ndoa walimpokea kwa bashaha Baba Mary.
Walikaa pamoja, yaani mume wa Mama Mary wa sasa ambaye wamefunga ndoa, Huyo mzazi mwenzie mama Mary ambaye ndie baba Mary halisi, Mary mwenyewe na Mama Mary walikuwa wanaongea na kucheka kwa furaha.

Baadaye mgeni wao (mzazi mwenzie mama Mary) aliaga na wote kwa pamoja akiwemo mume wa ndoa wa mama Mary walimsindikiza na kuagana kwa furaha.

Majirani wambeya wambeya tulikuwa tunachungulia tu na kufurahia amani iliyokuwa imetawala eneo lile na hasa kuona jinsi mume wa ndoa wa huyu mama alivyokuwa hana wivu, ni MNYAKYUSA na mama Mary ni Mzaramo, Baba Mary halisi ni Msukuma

Nawasilisha

Ulishasema nyie ni majirani wambea poleni kwa kukosa ubuyu wa kusambaza mtaani. Ukitaka habari za ndani kuwasimulia wenzako karibu nyumbani nikupe ubuyu faragha, ila uje peke yako.
 
Back
Top Bottom