Wanaume wa hivi ni hovyo

Wanaume wa hivi ni hovyo

64Bits

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
961
Reaction score
565
Leo naomba niwaongelee wanaume wenye tabia hii.

Hivi inakuwaje mfano mkeo/partner unae lala nae kitanda kimoja anakuamsha usiku anakwambia mpenzi naumwa unamtazama unamwambia "pole".

Kisha unageukia upande wa pili unalala mpaka asubuhi.Hujali hata kuuliza ni nini kinachomsibu mwenzio na unawezaje kumsaidia.

Ngoja sasa aumwe yeye, mtoto wa kike ataamka, atamtengenezea chai kama anahitaji hata supu atapika na ikibidi atamuogesha.

Hivi wanaume hamfikiriagi kuwa na wanawake nao wanahitaji huruma na ukarimu na kupendwa especially wakiwa hawasikii vizuri.

Kama mwanaume unavyojisikia raha ukiletewa kikombe cha chai kitandani ukiwa unaumwa basi na mwenzio atasikia raha vile vile ukimfanyia jema.

Haya basi kupika huwezi basi hata kauli laini huna, mpaka aumwe vipi ndo awe anaumwa sana mpaka umjali au mpaka akifa ndo utajua alikuwa anaumwa sana.

Mtu unapaswa ujifunze mwenzio anapenda nini kutoka kwenye yale mema anayokufanyia, ukimfanyia hivyo na yeye atafurahi. Baadhi ya wanaume wanadhani wakishatoa hela nyumbani then basi, hela ni za muhimu lakini sio kila kitu, wanaume wa hivi hovyo.
 
Kuna usemi unasema "u cannot change a man unless he is ready to change"!kuna vitu unatakiwa uchunguze tangia awali kwenye mahusiano na kama hujaridhika navyo usijipe matumaini kwamba utaweza kumbadilisha hivo vitu mwanaume umfinyage utakavyo.mfano kitendo cha kujali kinaendana na tabia ya mtu,kama unaona tangia mko kwenye urafiki jamaa sio mtu wa kujali usitegemee akujali mkifunga ndoa! kuna vitu unakubali tu na maisha yanaendelea!ijapokuwa nakuelewa sana coz i prefer the same nipate mtu atakayenicare nikiwa siko sawa kama mm ntakavyomcare!!
 
Haya mambo yanatokana zaidi na malezi. Mwenza aliekulia kwenye familia ambayo hakuna anaemjali mwingine na kila mmoja anajihudumia kama wanyama msituni, hawezi kuona umuhimu wa kujali na hata hagundui kwamba yeye amehudumiwa kwa upendo.

Una wajibu wa kumsaidia kubadilika. Ukiumwa asipouliza unaunwa nini muambie gently hujaonyesha kunijali. Muambie naomba chai, naomba unipeleke hospitali etc. Muda unavyozidi kwenda atajigundua na kuanza kufanya bila kuombwa. Ila kama wewe ni mtu wa kujali sana matendo ya upendo, usiolewe na mtu mwenye social status tofauti na yako. Utaishia kudekea waume ama wake wa majirani zako afu itakuwa mbaya.
 
Kinachowaponza wanawake ni tabia yao ya kudeka deka kama watoto wachanga..hasa wakijua kuwa unampenda na kumjali sana yaani atakufanya robotic machine..unaeza pigiwa simu kazini kuwa nyumbani kuna matatizo na ukaaga ukija resi unakuta kumbe mtu kajikata na kisu kidoleni wakati akikata kitunguu jikoni..unampa huduma ya kwanza huku unajisemea kimoyo moyo " sasa hili nalo ni la kuitwa mimi kutoka kazini au biasharani..?"....
Mtiririko wa matukio kama haya ndio yanayofanya muda mwingine tuwe tunawapuuzia hata kama mpo siriazi....lazima mtambue kuwa japo tunawapenda na kuwajali lakini vile vile na sisi huwa tumetingwa na makazi mengi na kupata uchovu wa ajabu...na tukipata nafasi ya kupumzisha mwili huwa tunapumzika....kama ukijihisi kichwa kinauma chukua panadol umeze na maumivu yakizidi ndio uniamshe...sawaaa...??
 
Back
Top Bottom