Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,468
- 119,622
Habari ya weekend wakuu,
Leo bwana kwenye daladala ya huku kwetu gomz kimetokea kisa kimoja.
Aliingia kwenye daladala mama mwenye mtoto na siti ya mbele kabisa karibu na mlangoni alikaa m'baba kwa kumuangalia anaweza kuwa yupo mid/late 40s.
Kando yake alisimama mwanaume mwingine wa makamo yaleyale, basi yule aliyekaa akasimama kumpisha yule mama akae.
Aliposimama akaanza kumwaga povu (kumbe alikuwa ameambiwa na yule aliyesimama kuwa amsaidie mtoto ).
Wacha ateme povu eti ooh wanawake hampendani, mwenzenu anaingia mnashindwa kumpisha kwa sababu gani? Mwenzie akawa anamtuliza, walikuwa hawajamuona si unaona gari imejaa?
Ye kakomaa hamna walikuwa wamemuona wanawake wana roho mbaya sana, yaani hawapendani kabisa.
Kusema kweli yule mama aliyeingia na mtoto mimi sikumuona maana nilikuwa nimejilalia zangu usingizi, na hata ningemuona nisingempisha bali ningempokea mtoto.
Ila yule baba mimi kanishangaza sana, ni kwa nini anadhani sisi wanawake ndio tunatakiwa kupisha?
Kwanza yeye alikuwa jirani kabisa pale kwa hiyo badala ya yeye kupisha alitaka atokee mwanamke aliyekaa nyumba ndio apishe?
Niwaulize ninyi wanaume, hivi akiingia mama mwenye mtoto au mjamzito anayetakiwa kuwa wa kwanza kunyanyuka kwenye siti ni ninyi au sisi?
Yaani sisi tunabeba mimba miezi tisa, tunalea hadi watoto wanafikia umri wa kujitegemea eti inapotokea tupo huru yaani hatuna mimba wala mtoto wa kunyonyesha bado tuna wajibu wa kuwapisha wenzetu walio katika hali hizo?
Kweli leo nimejua kuwa ni shughuli pevu kuzaliwa mwanamke Afrika, nadhani wanawake wa Afrika tuna mbingu yetu spesho maana sio kwa kazi hii tuliyonayo.
Nilitaka nimtolee uvivu yule mwanaume ila nikaamua nikae kimya maana nilikuwa na my uncle mmoja naheshimiana nae na anajua mimi siongeagi kabisa
nikaamua kuilinda image yangu
Hebu tuoneeni huruma
NB: Hapa nazungumza na wale ambao huwa wanapisha sio wale makauzu

nikaamua kuilinda image yanguHebu tuoneeni huruma