dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,475
- 2,078
Hahahaaa, Najua ni ONYO.Nzi anayetaka kufia ndani ya glasi ya bia
Asante kwa 'kuja'-li
Hahahaaa, Najua ni ONYO.Nzi anayetaka kufia ndani ya glasi ya bia
Tatizo unaweka kambi,Cheps nyingine nuksi tupu. Ukute hata ladha hana unajikaza kiume lakini ndo anataka kumpindua bi mkubwa home
Chepuko nuksi ujiloge umtie mimba ndo balaa mpaka Trump atajua.

'Status' na Majukumu/Uwajibikaji Lakini ujue.Kwa hiyo mchepuko ndo unaokupa raha.mkeo hakupi raha.loh same time kuolewa ni kuhousegirlika tukha jamani wanaume nyie.Ambae Hana mchepuko aje hapa mm sitaki kuolewa.![]()
Hivi mkuu unakaa pande zipi!!. .. Mana daah una maneno mpaka nashangaa...Kila side chick anatamani siku moja awe main chick, tena hawa ambao uliwambia Iam married halafu wanajifanya mioyo yao imetengenezwa na maganda ya bamia, anakwambia "worry not darling mi sinaga hata wivu wala sitakubana ila tu nikikutaka unipe dyudyu yangu usijifanye bize na mkeo am ready for wateva"
Ndo wana balaa sio mchezo mkianza atajifanya anamheshimu mkeo kabla ya kupiga simu anakuuliza 'are u free nikupigie' ila baadae dyudyu ikikolea anasahau (baundary) basi anajikurupukia tu sa9 usiku anatwanga eti "nimekuota bebi i wish you were here"
Mhh saa hizii? Akiona hukolei sasa anakutengenezea balaa ili mkeo agundue, akikukosa kwenye lipstick kwenye kola ya shati basi siku hizi wana misabuni yao na viungo- mseto vya kuweka ndani ya uvungu kunogesha penzi vinanukia balaa vinaitwa mishki na shaibu.
Nyuchi zinawekewa pilipili hoho mixer na viungo vya pilau mzee ukichepuka ukirudi home mkeo lazima agundue maana unabakia na harufu ya biriani siku 3 hata uoge na OMO haitoki labda ujisugue na utomvu wa mpapai na steel wire.
Mchague mmoja kati ya hao ulowamention then atakudadavulia kiroho sayona
Bora urudi tu kama mwana mpotevu, kuliko kuangamiaMichepuko sina hamu nayo kabisa, yaani ina bajeti kali kuzidi hata hii ya kuhamia Dodoma, fikiria mchepuko eti unataka hela ya matumizi ya kila siku, mchango wa harusi (ndugu&marafiki). Ghafla unadai hauwezi kupanda bajaj kila siku unataka gari.. Mi ngoja nirejee kwa mke halali wa ndoa. Hizo hips za mchepuko kama dili azile basi.
Mkuu ulifanya jambo la maana. Nilishawahi kuwa na michepuko kadhaa, nianze na Maureen yeye alikuwa muuza duka la Nguo, kila akikupigia simu yake ujue ni kizinga cha haja. Kuna siku alinipigia eti kapata loss ya laki 3 dukani anaomba nimlipie nikamtumia laki 2, kesho yake akanipigia dear upo wapi? Nikamuambia nipo Arusha kikaz akadai nna hamu ya kukuona nikamkatia tiketi ya fastjet 230,000 (return ticket) sasa siku ya safari nakumbushia awahi airport eeh anadai eti kapata period (tumbo la hedhi) kalala hawezi kusafiri aisee nilipata hasira. Nikamblock na kufuta namba yake. Michepuko ni ugonjwa wa moyo.ila kiukweli wanaume hatuwatendei haki wake/wenza wetu, kuna siku hiyo side chick alikuwa anataka pesa sijui akasuke na kupata pesa ya kununulia nguo eti kuna sherehe ya bethidei ya shoga yake ili atokelezee, akaomba kama laki hivi. Namnukuu "baby naomba laki tuu si unajua kuna party ya fulani nataka nitokelezee" nikamsikilizaaaaa katika hiyo simu alopiga, alipomalipomaliza kuongea sikumjibu, nikakata simu, kisha nikakaa na kuanza kufikiria. Maana juzi kati tuu mama mwenye nyumba alitoka kuniomba pesa ya kufanya shopping na pocket money ya matumizi ya hapa na pale, nikamtoleaga nje kuwa sina pesa.
Aisee baada ya kukata simu ya huu mchepuko simu na kufikiria kwa muda, nikainua simu na kumpigia maza haus na kumwambia, ombi lake limesikilizwa. Nikirudi nitampatia kiasi alichoomba. Aisee niliporudi tuu home, nikakata kilo 2 na kumkabidhi fanya unachotaka kama ulivyoniambia. Aisee alishangaa, maana sijawahigi kumpa pesa kama hiyo kwa mkupuo. kesho yake narudi home nakuta kuna mchele, mafuta, unga maharagwe na mazagazaga mengine ya jikoni. Huku yeye akiwa kanunua gauni moja na mimi kanichukulia shati moja kama suprise. Aiseeee nilijiona nimeokoka katika mdomo wa mamba mchepuko.
washenzi sana hawa michepuko, Ila na sisi wanaume tunayatakaga haya matatizo ya michepuko.
Hahahahahahahila kiukweli wanaume hatuwatendei haki wake/wenza wetu, kuna siku hiyo side chick alikuwa anataka pesa sijui akasuke na kupata pesa ya kununulia nguo eti kuna sherehe ya bethidei ya shoga yake ili atokelezee, akaomba kama laki hivi. Namnukuu "baby naomba laki tuu si unajua kuna party ya fulani nataka nitokelezee" nikamsikilizaaaaa katika hiyo simu alopiga, alipomalipomaliza kuongea sikumjibu, nikakata simu, kisha nikakaa na kuanza kufikiria. Maana juzi kati tuu mama mwenye nyumba alitoka kuniomba pesa ya kufanya shopping na pocket money ya matumizi ya hapa na pale, nikamtoleaga nje kuwa sina pesa.
Aisee baada ya kukata simu ya huu mchepuko simu na kufikiria kwa muda, nikainua simu na kumpigia maza haus na kumwambia, ombi lake limesikilizwa. Nikirudi nitampatia kiasi alichoomba. Aisee niliporudi tuu home, nikakata kilo 2 na kumkabidhi fanya unachotaka kama ulivyoniambia. Aisee alishangaa, maana sijawahigi kumpa pesa kama hiyo kwa mkupuo. kesho yake narudi home nakuta kuna mchele, mafuta, unga maharagwe na mazagazaga mengine ya jikoni. Huku yeye akiwa kanunua gauni moja na mimi kanichukulia shati moja kama suprise. Aiseeee nilijiona nimeokoka katika mdomo wa mamba mchepuko.
washenzi sana hawa michepuko, Ila na sisi wanaume tunayatakaga haya matatizo ya michepuko.