wa zion
JF-Expert Member
- Mar 23, 2013
- 222
- 476
Jamii tunayoishi kwa asilimia kubwa inaamini uzazi wa mpango ni kwa ajili ya wanawake tu, kumekua na changamoto nyingi sana pale wanaume wanapoambiwa wao pia wanaweza tumia njia ya uzazi wa mpango ambazo hasa ni tatu tu ikiwa ni kutumia Kondomu(njia hii hutumika kwa wengi kwenye kujikinga na magonjwa hasa hasa na si mimba zisizo tarajiwa), kufunga uzazi, na kutumia kalenda.
Je wewe kama mwanaume unaweza funga kizazi kama njia ya uzazi wa mpango baada ya mke wako/ mchumba? Je kuna wanaume ambao tayari mmeshafanya hivyo?
Wanawake mngependa wanaume wenu watumie uzazi wa mpango au mtaendelea tu wenyewe?