Wanaume tukome kuwekeza kwa mahawara!

hiyo ni msg tu.je angekua amempa hela?nyie wasichana mnasema wanaume ni waongo ndo maana nasema hivi alkuwa anamdanganya ili amchome tu basi.au ni mladi wa mwanaume ambao ameamua ampe hawala wake ausimamie coz huyo mwanamke wake wa nyumba kubwa haaminiki.kwa ufupi hiyo nyuma hakuna maelewano.wanawake wenye akili hawakagui simu za wapenzi wao ili kulinda ndoa.mia
 
"Tujihadhari na tujiepushe na zinaa kwani ni nuksi kubwa na inaleta ufukara,na unaivua imani yako kama unvyovua nguo,jee uko tayari kujiona watembea uchi@basi hivi ukifanya ni sawa na unaetembea uchi mana unaivua imani na mwisho utajikuta ni ibilisi huna ulichobakiwa nacho stara ishakuondoka.
tuache zinaaa
tuogope zinaaa
tuikimbie zinaa
tujiepushe na zinaa
tuusiane kuhusu uchafu wakuzini
tumuogope M.Mungu na moto uwakao kwa ukali."
Source: Mimba Kabla Ya Ndoa - Zanzibarwebsite
 
Kwa kweli wanao fanya haya hasa huwa ni wame za watu siku ukiwa huna kitu kwa hao mahawara unapisha wenzio wenye nacho waendeleze kula vyombo wanawake wengi wa nje wanaangalia pochi yako tu coz hawahitaji kupiga picha na wewe ipo siku na yeye huyo mwanaume ataumizwa mara mia ya anavyo muumiza mkewe.

Nimeona sana wanaume wa stly hiyo huwa mwisho wao ni mbaya na huishia kupata haibu tu kwa jamii . Hembu jaribuni kuwaambia hao mahawara umepata tatizo na mambo yako ya kifedha hayaendi vizuri uone nakupa week tu utapata majibu hakuna cha baby wala swtheart utasikia tu ili nalo lisumbufu na utaishia kutopokelewa simu kabisa . Cha muhimu tulieni kwenye ndoa jamani unaepuka mengi sana

tawele.tumekusikia mama.
 
"Tujihadhari na tujiepushe na zinaa kwani ni nuksi kubwa na inaleta ufukara,na unaivua imani yako kama unvyovua nguo,jee uko tayari kujiona watembea uchi@basi hivi ukifanya ni sawa na unaetembea uchi mana unaivua imani na mwisho utajikuta ni ibilisi huna ulichobakiwa nacho stara ishakuondoka.
tuache zinaaa
tuogope zinaaa
tuikimbie zinaa
tujiepushe na zinaa
tuusiane kuhusu uchafu wakuzini
tumuogope M.Mungu na moto uwakao kwa ukali."
Source: Mimba Kabla Ya Ndoa - Zanzibarwebsite

wasikurubie zinaa
 
Hii topic imenikumbusha vituko vya baba yangu. Baba yangu alikuwa ni mfanyabiashara. Kwa hiyo alikuwa anajulikana sana kwenye mabenki, those days ni hizi benki za serikali. Sasa alikuwa hajatulia though yeye alikuwa a bit smart in a sense hakuwa na hawara ambaye anaweza kujiita nyumba ndogo ni alikuwa ni kind of hit and run.

Sisi tulizaliwa wengi (wote mama mmoja baba hakuwahi kuzaa nje). Mama alikuwa akisafiri baba analeta wanawake ndani akitoka kwenye pombe zake. Kuna kipindi alikuwa anamleta mdada mmoja mfanyakazi wa benki; those days wadada wa benki walikuwa warembo sana na walikuwa wanapenda saaaana ma sugar daddy. Sasa kwa kuwa dingi alikuwa corporate customer alikuwa anawapata kirahisi.

Ndugu zangu wakaweka kikao (mimi nilikuwa mdogo sijuhi std two vile wao walikuwa a bit old, walikuwa secondary) Wakapanga kuwa baba akimleta hawara yake wamfundishe adabu.

Baba yangu hajawahi kulala nje nadhani ndio maana alikuwa anaamua kuwaleta wanawake ndani afu wanaondoka asubuhi sana kama walinzi, na yeye alikuwa ana imani kuwa hatumuoni kwani alikuwa na funguo zake na geti alikuwa anafungua mlinzi.

Siku moja karudi na mwanamke wake kama kawaida yake dada zangu na kaka zangu walikuwa wamejificha kwenye maua na fimbo zao; walishamsoma akiingia anamshusha huyo mwanamke , afu yeye anaingiza gari garage, ndio wanaingia wote ndani. Ile anaingiza gari garage wacha ndugu zangu waibuke na kuanza kumtandika yule mwanamke. Alipiga makelele, nadhani pombe zilimtoka. Ilibidi baba achukue gari alimrudishe yule dada. from that day hatukuwahi kuona mwanamke yeyote home na baba hakuongea kitu.

Mama alivyorudi wote tulikaa kimya hatukumwambia what happended.

Hope none of my bro or sis is JF member. Maana atacheka saaana.

hii kali sana aisee,lakini du Mkuu,mashine ya mzee mkaicharanga bakora? Angewafia je?
 
Mambo ya mpango wa kando ni mabaya sana, na ukikaa kifala unagezwa ***** mtozeni a.k.a ATM nyumba ndogo nooouuuumar
 
Mambo ya mpango wa kando ni mabaya sana, na ukikaa kifala unagezwa ATM. nyumba ndogo nooouuuumar
 
Hahahaha! Naogopa dhambi jamani..lol watoto wale dagaa afu mimi ninunuliwe draya?..khaaa sio laana ni nini husni? Jiulize hv je kama ndo mimi watoto wangu wanakula dagaa ntafurahi? Hizi nyumba ndogo hizi, zipo kwaajili ya raha tu, nyumba kubwa ndo za kuvumilia shida! Mume akisema wife nimeishiwa mwezi huu itabidi unihelp kulipa skuli bus, tunaitika sawa mume wangu, kumbe mwenzio hajaishiwa wala nini, hela zipo ila hazitoshi kugawana na hawara..

kinamama mbona hamnijibu,hakuna mdada humu mmu ambaye ni hawara wa mtu?
 
hiyo ni msg tu.je angekua amempa hela?nyie wasichana mnasema wanaume ni waongo ndo maana nasema hivi alkuwa anamdanganya ili amchome tu basi.au ni mladi wa mwanaume ambao ameamua ampe hawala wake ausimamie coz huyo mwanamke wake wa nyumba kubwa haaminiki.kwa ufupi hiyo nyuma hakuna maelewano.wanawake wenye akili hawakagui simu za wapenzi wao ili kulinda ndoa.mia

au vipi mkuu? Si unajua tena madhara ya chokonoa chokonoa?
 
Hakuna atakaye kujibu kwakuwa it's nothing to be proud of. Ndio maana hata kutembelewa ni mida ya night kwa kujiiba iba.
Wahusika wote ke/me nadhani nafsi huwa zinawasuta ni shetani tu kawapandia wanashindwa ku control tabia zao; but deep inside wanajua wafanyacho ni kitu kibaya.
kinamama mbona hamnijibu,hakuna mdada humu mmu ambaye ni hawara wa mtu?
 
Mambo ya mpango wa kando ni mabaya sana, na ukikaa kifala unagezwa ***** mtozeni a.k.a ATM nyumba ndogo nooouuuumar

lakini ndo hivo kila kukicha watu 'wanawekeza' kwenye small house,kina mama wanapiga kelele weeeeee but where!
 
Hakuna atakaye kujibu kwakuwa it's nothing to be proud of. Ndio maana hata kutembelewa ni mida ya night kwa kujiiba iba.
Wahusika wote ke/me nadhani nafsi huwa zinawasuta ni shetani tu kawapandia wanashindwa ku control tabia zao; but deep inside wanajua wafanyacho ni kitu kibaya.

hahahahaa lakini ya kwetu kinababa mbona tunakiri humu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom