Ama kweli, bora ukose mali upate akili!

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
WALIOSEMA bora ukose mali upate akili hawakukosea kuna wengi wanateseka kwa vile wamekosa uelewa wa nini wafanye ili waishi vema.

Kuna watu wanaishi maisha yasiyo na raha kwa sababu wanaumizwa na fedha zao, kuna watu wanaishi maisha magumu kwa sababu hawana fedha.

Wapo watu ambao kwa namna wanavyoishi, hakuna dalili kwamba hatma yao itakuwa nzuri. Kwanini kwa sababu utakuta labda mtu hajali maisha yake kwa kufanya vitu visivyo na maana.

Je wewe maisha yako yanafafanaje? Ama kweli bora ukose mali upate akili! Kurudi nyumbani usiku wa manani kwa sababu umetoka kulewa ni dalili kwamba maisha yako hayako sawa.Mwenye usawa ni yule ambaye anaishi kwa malengo, sio kuendekeza vitu ambavyo havimsaidii. Je wewe ukoje?
Tayari umeshaoa na unaendekeza ngono nje ya ndoa ni dalili kwamba akili yako ni mwezi mchanga (haijakomaa). Kuna wanaume wanajali zaidi mahawara na kudharau wake au watoto wao, hii si akili.

Mwanaume yeyote mwenye akili ya namna hii maana yake ni kwamba akili yake imeoza kwani kuna wengine ukinanihii nao wanatoa dhahabu, mbona unakuwa na akili mbovu ndugu yangu? Hata kama, ni vizuri kuwa na hekima. Ishi na wote kwa heshima. Ulimpenda mwenyewe, mbona sasa mmekuwa mnafanyiana mabaya? Acha hizo, fanya mambo ambayo wewe ukifanyiwa utajisikia amani.

Wanaume tukome kuwekeza kwa mahawara! Kuna wengine sura zao zimejaa hekima, matendo yananuka zaidi ya kinyesi, mke anampiga, watoto hawasomishi, yeye na makahaba. Gari lake hata mkewe haruhusiwi kupanda, wenye kupanda ni makahaba zake tu!
Kuna jamaa mmoja alifumwa na mkewe kwenye simu katumiwa ujumbe kutoka kwa kahaba ambaye alimuandika kwenye simu kwa jina la mjomba mkubwa. Meseji yenyewe ilisema
Mpenzi leo nimepita madukani Mbeya mjini. Bei ya vifaa ni hizi: Stima (500,000), Draya (400,000), Stima ya fasho (200,000), viti (60,000) na sinki la kusafishia nywele (600,000.). Fanya hima mpenzi kesho unipatie hizo pesa maana nasikia bei karibu zitapanda.Ukinipa milioni mbili na nusu zitanitosha na kununulia dawa za kuanzia mmwwaaaa nakupenda sana ikamalizia hiyo meseji.
 
Tatizo lipo hapa....

  1. Ndoa.
  2. Kucheat.
  3. Nyumba ndogo.
Majority wanaliangalia kwa "Black" and "white"...
Pale tu watu wa namna hio watapoanza kuangalia
the above in shades of "grey" tena a lot of shades of
"grey" then maybe tutaanza kuyajadili kimsingi zaidi.
 
kwani wanaume huwa mna akili sasa ? mbona maboya ni wengi tu humo kati yenu wengi sana sana
nimeona wengi anakopa anaenda kumnunulia hawara gari na nyumba .gari yenyewe anatumia mdada na mpenzi wake na nyumbani wanalala wote
 
Mbona huyo mwanaume sioni ukimpa majina kama unavyowaita hao wanawake mahawara..makahaba???Au yeye ndie anafuatwa na hao wanawake na kulazimishwa kutoka nje ya ndoa yake???

Nwy pole maana ulivyoandika kwa hasira ni kama yamekukuta....

Lizzy nashukuru umeliona na ww Sijui lini thaman ya mwanamke itapatikana tangu mwanzo wa sred anamwongelea ubaya wa mwanaume kwa kutumia jina sahihi kafika kwa mwanamke ambaye yy ni victim tu hapo cheki majina aliyotumia,wakati hapo mtendaji mabaya aliyestahili majina mabaya ni mwanaume lkn hajathubutu sijui bila huyo bazazi kahaba angetokea vp lol!
 
Lizzy nashukuru umeliona na ww Sijui lini thaman ya mwanamke itapatikana tangu mwanzo wa sred anamwongelea ubaya wa mwanaume kwa kutumia jina sahihi kafika kwa mwanamke ambaye yy ni victim tu hapo cheki majina aliyotumia,wakati hapo mtendaji mabaya aliyestahili majina mabaya ni mwanaume lkn hajathubutu sijui bila huyo bwana kahaba angetokea vp lol!

nafikir na ww unafanya kosa la alie tangulia, mpe jina huyo mwanaume km lipo
 
Back
Top Bottom