natumai wote m salama...
kuna mambo mengi wanaume tunayafanya ili kuonyesha umaarufu wetu wa kiuanaume ila mengine yanakera..kati ya mambo haya ni hili la kujipiga kifua kwa kufanikiwa kumega tunda la mwanamke au wanawake fulani..ila si uungwana kabisa kusimulia kwa kila yeyote kuwa umefanikiwa..hivyo basi nawaulizeni wanaume tuwache hii tabia ya kiuvulana..kama hujalala na mwanamke fulani,wacha kutangaza umelala naye,na kama kweli umefanikiwa kulala naye,wacha kutangaza umelala naye...ndiyo uanaume..
naombeni kuwasilisha ili tupate kupeana maoni katika suala hili..asante...kina dada pia tunataka maoni yenyu hivyo mnakaribishwa