Wanaume tubadilike, tuache tabia ya kuzaa na kutelekeza familia

Mr PJ

Senior Member
Jul 1, 2018
102
203
Hakuna kitu kibaya kama kutelekeza familia. Jana nimepata kukutana na dada mmoja amezaa na jamaa flani huyo jamaa ana kazi nzuri tu ila ukimcheki Dada mwenyewe kachoka kweli hata kazi anayofanya ni shida tupu.

Ukimuuliza anasema jamaa amemtelekeza yeye na mtoto, pamoja na kuwa na hela lakini hajali kabisa mtoto wake.

Hivi mtu kama unaweza kuwa na mahusiano naye kwanini ushindwe kulea mtoto wako au hata mama mtoto ukamtafutia kazi ya maana ili amtuze vizuri mwanao.

Utasikia tukijisifu vijiweni kwamba nina mtoto wangu yupo na mama yake sehemu flani ila hujui kama kala, kavaa ama anaishi vipi.

Tuache hii tabia mazee tunajiwekea laana ambazo hazina msingi mwisho wa siku unatafuta maisha hufanikiwi kumbe ulidharau vitu kama hivi.

My advice: Hakuna mimba ya bahati mbaya ukishaamua kulala na mtu na unajua hukutumia kinga no way out for the consequence.

Jiandae kulea, kuzaa zaa na kuwaachia wanawake walee tu sio uanaume wala wazazi/wazee wetu hawakua hivyo ndio maana walifanikiwa kuwa na familia bora.
 
Ni sawa, ila je kama sababu ya kufanya hivyo ni mama wa mtoto? Yaani mwanamke uliyezaa naye?

Hujakutana na vichomi wewe ukimlea mtoto anakulaumu na bado ukimwambia akuachie umlee wewe hataki anamnga'ng'ania

Kila jambo lina sababu, sio wanaume wote ni Maboya na hawapo responsible.

Uliza kwanza kwanini yatokee hayo?
 
Na je kama sababu ya kufanya hivyo ni mama wa mtoto? Yaani mwanamke uliyezaa naye?

Hujakutana na vichomi wewe ukimlea mtoto anakulaumu na bado ukimwambia akuachie umlee wewe hataki anamnga'ng'ania

Kila jambo lina sababu, sio wanaume wote ni Maboya na hawapo responsible.

Uliza kwanza kwanini yatokee hayo?
Kwanini uzae naye hali unajua ni kichomi?
 
Ni sawa, ila je kama sababu ya kufanya hivyo ni mama wa mtoto? Yaani mwanamke uliyezaa naye?

Hujakutana na vichomi wewe ukimlea mtoto anakulaumu na bado ukimwambia akuachie umlee wewe hataki anamnga'ng'ania

Kila jambo lina sababu, sio wanaume wote ni Maboya na hawapo responsible.

Uliza kwanza kwanini yatokee hayo?
Kweli watu wanatofautiana ila nenda hata ustawi wa jamii kuhakikisha mwanao anapata kile unachokitaka. Lkn mwisho wa siku kwann uwe na mahusiano na mtu ambaye unajua haeleweki. Kumbe bora kuacha ngono.
 
Kama umeshakuwa kwenye mahusiano utafahamu kuwa watu wanabadilika

Unaweza kuwa kwny mahusiano na Mwanamke mwanzoni asiwe na tatizo akaja kuwa tatizo baadae baada ya kuzaa nae.
 
Hayo Mambo mbona yanarekebishika?
Kila mmoja ana madhaifu yake,
Kwahiyo akileta ukichomi ndio umuache pasi na kumrekebisha?
Utaacha wangapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikiliza, yapo ya kuvumilia na kurekebisha...mengine hayafai

Kwa mfano, kama amepata Mwanaume mwingine kwa siri na akapata kiburi na hataki kuachana nae utamrekebishaje hapo?
 
Back
Top Bottom