Tunamshauri arudiane na mkewe: Waliachana baada ya mume kuzaa nje ya ndoa

Moronight walker

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
3,105
4,635
Ilikuwa miaka 5 iliyopita kaka yangu upande wa Baba mkubwa. Yeye alikuwa na ndoa yake kabisa na alikuwa na watoto 2 wa kiume na wa kike. Kaka yangu yule ni mtu wa ubabe ubabe.

Sasa miaka 5 iliyopita bro wangu alikuwa na mchepuko, sasa katika kuchepuka nae, yule dada alibeba ujauzito wake. Bro alikaa kimya tuu ampaka kujifungua mtoto wa kiume. Mtoto akufananae, mchepuko akamwambia kuwa mtoto ni wako. Bro akaona fresh tuu.

Sasa si unajua sisi wanaume unaona hile ni damu yako, bro akaamua kwenda kumtambulisha kwao na ndugu zake. Bila mkewe kumwambia.

Mtoto alipofikisha miezi kama 6 hivi aliamua kwenda kumwambia mkewe, sasa kosa alilolifanya alikwenda kibababe sio kwa upole na kutanguliza msamaha kwa mkewe kwa sababu alikuwa kachepuka na kupata mtoto.
Yeye alienda tuu akamwambia kuwa nilichepuka na kupata mtoto, ni mtoto wangu siwezi mkana na kumtupa na ninataka wazoeane na wanagu wa huku. Sasa kama wewe mkewe wangu hutaki basi wawezo ondoka au tukaachana. Hii ni damu yangu siwezi itupa.
Ni makosa aliyofanya kaka yangu yule.

Mkewe ni mtoto wa Kimburu tena msomi anamasters na kazi yake na mambo yake mengine.

Maneno yale yalimchukiza shemeji na kugombana sana tena sana. Ila mwishowe waliachana , shemeji yeye ni mtu asiyependa dharau sana, na aliona kama mume kadharau flani hivi ila ni long story. Walifanikiwa kuachana na walijenga nyumba moja kubwa sana japo haikuisha ile nyumba iliuzwa na kugawana kila mtu chake.

Sasa mwaka jana mwishoni yule mchepuko wake alimchukua mtoto akaenda nae dodoma, yule mchepuko akamwambia tuu baada ya kufika dodoma kuwa samahani sana huyu mtoto sio wako. Nilifikili ni wako ila ni wa ex wangu mmoja kwa sababu amefananae. Samahani sana kwa yote yaliotokea.

Sasa bro akabaki na mshangao ikamlazimu kwenda nyumbani kwao kwa wazazi wake ili kupata data, alikutana na mdogo wale Akamwambia kuwa kipindi yupo nae alikuwa pia anatembea na mtu mwingine ambaye ni Baba mtoto.

Ila alipopata ujauzito alijua ni wako , na mtoto alivyozaliwa alijua ni wako, kadili siku zinavyoenda hasa baada ya miaka 2 mtoto akaanza kubadilika na kuwa anafanana na ex wake huyo. Ila alikaakinya tuu , sisi hapa home huyo kaka tunamjua , sisi wenyewe pia tulishituka pia, japo dada yangu alikaa kinywa kwa muda mrefu. Mdogo wake alimuonyesha picba ya jamaa na bro alisema kuwa ni kweli kafanana na mtoto kabisa.

Yule dada kwa sasa yupo dodoma kwa Baba mtoto, ila huyo jamaa kamwambia kuwa atamrudishia gharama za kusaidia kumtunza mtoto mpaka kufika miaka 5, kama kufidia pamoja na kumlea mtoto. Sasa sijajua ni ngapi waliamua wenyewe.

Sasa kumbuka ndoa ilivyunjika, mimi now nipo rwanda narudi next week nimeona kwenye group la familia wakimshauri kuwa aongee na ex wife wake warudiane.

Hii ishu wadau, ushauri tafadhali.
 
Zuzu kivipi mkuu
Kiuhalisia hawezi kumdharau mke wake kiasi kile.
Watu wengi sana(wanaume na hata wanawake) wana watoto nje ya ndoa.
Lakini wanatunza siri isijulikane hadi wamekuwa watu wazima.
Hii kumuonyesha mke wako kuwa wewe ni kijgoo na umezaa nje, na huna la kujutia, hilo linamweka kaka yako katika mtego alioingia mwenyewe.
Mwanamke kurudi kwake atafanyiwa hivyo hivyo tena.
 
Kwa kweli wahenga walisema usiache mbachao kwa msaala upitao. Siku zote huwa nasema hakuna mchepuko anayeweza kukutakia wema wanaume huwa hawajifunzi. Unamdharau mkeo mwisho wake ndo hayo. Ametaka yote kwa pupa amekosa yote.

Aende kuomba msamaha ajaribu bahati yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi Wairaqw hatupendi dharau kabisa. Mkewe atakua ameshamove on na sidhani kwa misimamo tunayokuaga nayo ataweza kumpokea kama mume tena. Kama ni makosa aliyashayafanya angekutumia tu busara kwa mkewe ila ubabe plus dharau shida ndo ilipoanza. Kama deep down amejutia anaeza kujaribu kutumia wazee wamuombee msamaha probably mkewe bado anampenda.
 
Nadhani ni vyema na kule upande wa mwanamke waunde group lao nao wamshauri mwanamke kisha group zote mbili ziungwe zilete mrejesho kisha wasubiri maamuzi ya wahusika maana wao ndo wanaujua utamu wao waliokuwa wanapeana
 
Back
Top Bottom