Wanaume tuache kuwa Watumwa kwa wanawake

Bwana misitu

Member
Aug 1, 2014
40
94
Habari za muda huu wanajamvi!.

Wanaume wenzangu kichwa cha habari hapo juu chakusika.

Wazee mimi nina jamaangu tumefahamiana ni zaidi ya miaka 3 nyuma iliyopita, tunafanya kazi ofisi moja, tunasaidiana kimaisha na hali nyingine zakimaisha pale inapolazimu kufanyia hivo. Ila tofauti ni kwamba jamaa anaishi na mwanamke mimi bado nakataa ndoa kama ilivyo kauli mbiu yetu.

Ila kitu kinachonishangaza kwa huyu kijana mwenzetu aisee jamaa mwanamke anampelekesha kiasi kwamba jamaa yupo ndo kama kawekwa ndani na huyo dem, jamaa kitu chochote anachomwambia mwanamke lazima amtimizie, mwamba yupo tayari akope hata kwa riba ila sio amwambie mwanamke wake hicho kitu sina au vumilia kwa muda then ntakupatia.

Mbaya zaidi jamaa kila kitu kinachohusiana na job pale huyu mwanamke wake lazima amwambie yani mwanamke wake ni kama tu nae ni staff mwenzetu maana hakuna asichokifaham.

Kinachonishangaza zaidi mwamba hana maamuzi kama mwanaume kwanza kadi ya bank anamiliki dem yani hata mshahara ukitoka jamaa anaenda kuomba hela yakutumia kwa mkewe, hata akitaka kusaidia ndugu yake lazima aende kwa mkewe kueleza hyo shida ya ndugu yake halafu mkewe ndo ataamua kama huyo mtu asaidiwe au lah !

Mwanzoni mwa mwaka huu mwana alichukua loan kama 25M hv dem akamwambia ampe 15M akafungue duka la nguo sasa mm kidogo nikawa nimemjaza mwamba sumu aache uboya hiyo hela afanyie malengo yake kama alivyokuwa ameipangia huwezi amini dem kumbe alivyoona km jamaa anataka kusimamia misimamo mikali tuliyompa mimi na wadau dem akamwambia kama hunipi hiyo hela tuachane, Dah! jamaa alimpa dem 20M ili asiachwe.!! Bad enough nashangaa mshkaji anabembeleza nini wakati dem ni golikipa tu hana mchango wowote kwenye maisha ya jamaa na hawana hata mtoto kwanini asipige chini..!!

Wazee mimi binafsi na washkaji wengine pale ofisini tumejitahidi sana kumsanua mwana aache ufala ila mpaka saizi jitihada zetu zimegonga ukuta tumeamua kumtema andelee na ufala wake wakuwa mtumwa wa mwanamke..

Binafsi nimeamua kuileta hapa nipate maoni kwa wadau tofauti je ni sahihi mwana anavyofanya kwamba ndo mapenzi yeyewe au ni uboya dume lenzetu linaangamia kwa kukosa maarifa...

NAWASILISHA KWENU WAKUU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za muda huu wanajamvi!.

Wanaume wenzangu kichwa cha habari hapo juu chakusika.

Wazee mimi nina jamaangu tumefahamiana ni zaidi ya miaka 3 nyuma iliyopita, tunafanya kazi ofisi moja, tunasaidiana kimaisha na hali nyingine zakimaisha pale inapolazimu kufanyia hivo. Ila tofauti ni kwamba jamaa anaishi na mwanamke mimi bado nakataa ndoa kama ilivyo kauli mbiu yetu...

Huwezi kujua mwamba anapata nini mpaka kufikia maamuzi hayo....Nyumba zina mambo mengi.
 
Ni ujinga wa hali ya juu mwanamke kukupelekesha.

Yesu aliwahi sema tuwe watu wa " ndio" na pia " hapana". Lazima uwe mtu mwenye kauli, mwanamke akikupanda kichwani, unampiga chini, kwanini udhuru maisha yako, uchumi wako na future yako kisa mwanamke?

Tabia hizihizi zilimpelekea Samsoni kutobolewa macho.

Naunga mkono hoja.
 
Habari za muda huu wanajamvi!.

Wanaume wenzangu kichwa cha habari hapo juu chakusika...
Huyo rafiki yako bila kumungunya maneno kashapigwa kipapai, na Kuna uwezekano huyo mke wake ni mchawi au anatoka familia ya kichawi. Cha kufanya hapo ni kumsadia bila yeye kujua ili muweze kumuondolea aliyolishwa na kunyweshwa, matokeo yake kainamishwa kichwa.

Jamaa ukute hamjari hata baba yake huko kijijini. Yuko kifungoni mtoeni
 
Huyo rafiki yako bila kumungunya maneno kashapigwa kipapai, na Kuna uwezekano huyo mke wake ni mchawi au anatoka familia ya kichawi. Cha kufanya hapo ni kumsadia bila yeye kujua ili muweze kumuondolea aliyolishwa na kunyweshwa , matokeo yake kainamishwa kichwa.

Jamaa ukute hamjari hata baba yake huko kijijini. Yuko kifungoni mtoeni
Hata kwa uchawi haitakiwi upelekeshwe na mwanamke
Kwani huwa hamsali??
Sasa uchawi unakushikaje?
 
Back
Top Bottom