Wanaume tabia hii vipi?

Pia mleta mada ujichunguze unaweza kuwa ni sababu ya tatizo. Kuna wamawake wengine mmewe akifika nyumbani mwanamke anaanzisha kelele na visa hadi nyumba inakuwa haikaliki. Jichunguze na kama hauna tatizo mkalishe chini mzungumze mtoane kasoro na kurekebishana mwishowe tatizo litaisha.
Naamini asilimia 98 Sina tatizo, kumkalisha nimeshajaribu Sana labda naomba unisaidie mbinu nyingine tafadhar
 
Kabla hauja chukuwa uamuzi wa mbali anza kwa kuongea nae mweleze unacho taka au unavyo jiskia anaweza kuwa anajuwa umekubaliana na moves zake so ongeeni kwanza asipo tulia home lete feedback
 
wanaume ni wabinafsi sana ,wana roho mbaya kuloko shetani lea tu mwanao mamy ishi nae tu maisha yaende
we dada aliekutendaga kaleta balaa mana nakuona kila mahali unakandia wanaume....... sasa sijui sahv umekua lesbian au unakula dyudyu tu kimaslahi
 
Habarini wana mmu, Mimi Ni mwanamke ambaye nimeolewa na Nina Mtoto mmoja mchanga miezi 3,tatizo nililonalo Ni kwamba mume Wangu huwa hapend kukaa nyumbani yeye akirud kutoka Kazini Ni kupumzika kidogo then anatoka Hadi usiku Sana Hana muda Hata wa kunisaidia kukaa na Mtoto angalau nami nipumzike kidogo maana anajuwa jinsi Mtoto anavyosumbua na tunakaa wenyewe tu Mimi na yey mume Wangu,daima yeye anajali company za marafiki tu. je apo tabia hii inaashiria nini?mapenzi yapo kweli au ndio Sina changu tena?
Unataka mimba nyingine?
 
Naamini asilimia 98 Sina tatizo, kumkalisha nimeshajaribu Sana labda naomba unisaidie mbinu nyingine tafadhar

by the way....unasema upo mwenyewe umechoka kulea mtoto? Miss wa kuja jf kuchat unao wa kutosha ila kulea mtoto huwezi mpaka usaidiwe na mista sio?
 
Jaribu kujichunguza na upande wako pia. Wanaume hawapendi kelele wala dharau...

Vinginevo pata muda wa kuongea nae kumweleza vile unavotamani awe karibu na familia. Ukiongea nae kwa utulivu naamini atabadilika,hakuna mwanaume kichwa ngumu kwa mwanamke mnyenyekevu....
 
Siyo siri mi mwenyewe kukaa na mtoto mihani sana. Usijali mamii tupo wengi mumeo yupo kama Mimi hapa. Anakupenda wala usihofu
 
Jaribu kujichunguza na upande wako pia. Wanaume hawapendi kelele wala dharau...

Vinginevo pata muda wa kuongea nae kumweleza vile unavotamani awe karibu na familia. Ukiongea nae kwa utulivu naamini atabadilika,hakuna mwanaume kichwa ngumu kwa mwanamke mnyenyekevu....
Valentina safi sana wewe ni mfano wa kuigwa, umeshaolewa?
 
Vitu vingine bwana, kwahiyo unataka mumeo akirudi kazi yake iwe kubembeleza mtoto si ndiyo maana yako?
 
Vumilia tu kidogo, mtoto akifikisha miaka miwili hivi+ utakuja tena kusema mumeo anapenda kukaa na mtoto sana.
 
Jaribu kujichunguza na upande wako pia. Wanaume hawapendi kelele wala dharau...

Vinginevo pata muda wa kuongea nae kumweleza vile unavotamani awe karibu na familia. Ukiongea nae kwa utulivu naamini atabadilika,hakuna mwanaume kichwa ngumu kwa mwanamke mnyenyekevu....
We dada najikutaga napenda kusoma coment zako basi tu imetokea
 
kuna wanawake wakisha kuwa na watoto wanakuwa rafu rafu...wachafuwachafu sijui ni kuzidiwa na kaz ? wanaume hatupendagi.ndio maana hatukai nyumban
 
Back
Top Bottom