wanaume na tabia za ghadafi(rais wa Libya) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wanaume na tabia za ghadafi(rais wa Libya)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lokissa, Feb 23, 2011.

 1. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  WanaJF nimeonelea nianze na hii title ili nieleweke vizuri. Kwa wanomjua rais wa Libya anataka wanaompinga wauwawe ama kufungwa maisha na pia kawaita ni mende(komba mwiko),walevi,wavuta unga,magaidi nk.Kasahau kuwa watu hao hao wlaiokuwa wanamkubali wamemgeuka kwa sera zake mbovu na za kidikteta,anataka yeye ndio awe na sauti ya mwisho kwa kila kitu kinachohusu LIbya bila kujali athari zake.

  Nasema hivi kwa sababu wanaume wengi tuko hivo katika ndoa zetu.Wakati wa kuchumbia yawezekana ulikuwa na chumba kimoja tu tena cha kupanga na una kitanda kimoja na tv ya nchi 14 tu.Unampata mchumba yy kaamua kukuvumilia kwa jinsi ulivo yy hajali una nn bali anajali upendo wa dhati,kwa kuanza akakuletea jiko na sufuria na kukushauri usile magengeni.Baadae mkaoana na kwa kuwa kila mmoja wenu ana kazi mkaamua kupanga nyumba ya vyumba wiwili huku mkinunua kiwanja na kujenga kibanda chenu cha kuishi na pia kwa watoto mtakaojaliwa.Mungu kawajalia mkapata watoto wa 4 na mnashirikiana kuwasomesha.Sasa we mwanaume baada ya kukaa kwenye ndoa na kujiona sasa we ni kichwa cha nyumba ukaanzisha udikteta ndani ya nyumba,hela za matumizi hutoi kwa vile mke nae ana kazi, mke kaamua kujiongezea elimu huku unamsimanga na haumsaidii ada wala kutunza familia,na pia umeamua kuwa na wa pembeni ambae unampa matumizi yote.Mkeo akiuuliza helaza matumizi unaishia kumtia vibao tena mbele za watoto huku ukimtaka afungashe virago vyake aondoke kwani hana adabu wala heshima na unataka kumleta nyumba yako ndogo kwenye nyumba ulioshirikiana na mkeo kuijenga.Hivi kweli inaingia akilini/ nkisema wanaume tuna akili kama za Ghadafi ntakuwa nimekosea?Hii ni habari ya kweli wanaJF
  WanaJF nawasilisha.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ningesema wanaume ni viumbe vya ajabu sema ntakua na waonea wale ambao hawana idiology za ajabu!!
  Kusema ukweli wanaume wa aina hiyo ni washamba sana....badala ya kufurahia kujiendeleza kwa mkewe ndo kwanza anaanza vituko?
  Hao ni wale ambao kila kitu wanataka wao wawe zaidi...si ajabu roho inamuuma mke kasoma zaidi na inawezekana yuko juu kielimu zaidi ya mume sasa hivi!

  Na huyo dada mpaka apigwe vibao mbele ya watoto jamani??Mambo yakizidi ugumu bora atafute pa kwenda....kama ameanza kumpiga na asipobadilika soon ...anaweza akamfanya kilema siku moja!
   
 3. PEA

  PEA Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. kutufananisha na Ghaddafi! Hiyo kali kweli. Kimsingi sio tabia nzuri kabisa lakini na nyie wanawake mkiwa juu kielimu mna mambo yenu! But all in all bila kuangalia upande wa pili, nyumba ndogo sio suluhu ya matatizo kamwe
   
 4. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijui huu uzembe wa wanaume kubembeleza wanawake ulianzaje,
  mwanamke unahofia nini wakati baba ni kichwa cha familia.
  acha baba na awe baba wewe mwanamkee na uwe mama na si ujiweke kwenye nafasi ya juu zaidi yako
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu kweli hicho kidume chenye tabia hiyo ni kama mfalme wa wafalme Gadaffi, lakini kutufananisha wote na huyu mjamaa ni kutokututendea haki.....
   
 6. N

  Nyoka7simba40 Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kibinaadamu hali hiyo haipendezi ikiwa upande wa pili haujabadili mwenendo ulioanza nao,ingawaje pia c vizuri hata kama hamuelewani hatua kama hizo huongeza tatizo,suluhisho la hali hiyo ni kila mmoja kuongeza mapenzi na unyenyekevu kwa mwenzie kwani hata mwanaume akiwa kama huyo rais wa wapi sijui hana neno kwani hata simba hupakatwa kwenye mapenzi .
   
 7. V

  Vumbi Senior Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jamii ya wanandoa katika nchi zinazoendelea ( Nyingi zikiwa Africa na Asia) inapitia katika kipindi kigumu cha mabadiliko katika malezi na uendeshaji wa familia. Jamii nyingi za kiafrica na Asia mpaka sasa wanaume ndio wenye maamuzi ndani ya familia huku wanawake wakikandamizwa kwa kutokuwa na uamuzi wowote japo wao ndio wazalishaji au watendaji wakubwa ndani ya familia. Kutokana na kukandamizwa wanawake wameanza kudai fursa sawa jambo ambalo baadhi ya wanaume wanaona ni sawa na kupoteza nafasi zao za maamuzi ndani ya familia hivyo wanaume hao wakiona mwana mke anataka kufanya jambo litakalo mwezesha kujijenga kimaisha wana hofu na huwa wanatafuta njia ya kumkandamiza asifanikiwe. Mabadiliko haya ndani ya jamii yanachangamoto zake ambazo ni baadhi ya wanaume kuona wanapoteza nafasi zao za maamuzi au baadhi ya wana wake kuona ni kipindi chao cha kulipiza uonevu wa wanaume. Hizi changamoto zinachangiwa sana na elimu walionayo wahusika na mapato ya kila mmoja. Hili jambo litapungua baada ya jamii kuwa na elimu ya kutosha na kila raia kulimiki sehemu ya uchumi uliopo bila kujali jinsia.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  dah,gadafi yupo juu jamani,
   
 9. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Pole Lokisa inaonekana yameshakukuta wapo wanaume wa aina hiyo ambao hata uwe mvumilivu wa kiasi gani huwawezi hapo swala mwanaume wa aina hiyo ni kumkanya asiposikia muitie wazee asiposikia ni talaka tu maana matumizi hatoi, penzi limehamia nje, wa nini sasa
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  thanks wadau mm ni mwanaume na kweli nimeshuhudia haya,si waume woye tuko hivo ila wengi wako hivo,
   
 11. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kila upande una mapungufu yake....kuna wanaume ni wakatili na kuna wanawake wanachangia wanaume kuwa wakatili kwa matendo yao....
  the issue is we should not take for granted what holds us together.......
   
 12. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  inaumiza sana!! mama akifikiri awaache watoto wake, roho inauuma unakuta anaamua kuvumilia vituko vya mumewe, wkt mwingine wanawake wanapigwa mpk wanatolewa vizazi!!
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kweli Susy inabidi kuwa makini na wachumba wa muda mfupi then mnaoana bila kujua walau nusu ya tabia zake, na pia kwa ushauri wa bure wanawake wajaribu kujiwekea akiba bila waume kujua jaribu hata kujenga kibanda chako mwenyewe taratibu usikubali mume ajue kikishakamilika andika hata jina la mwanao na pangisha ili siku mambo yakienda kombo usihangaike kuteseka sana.
   
 14. R

  Rinsa Member

  #14
  Feb 24, 2011
  Joined: Dec 13, 2007
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wajaribu kujiwekea akiba bila waume kujua jaribu hata kujenga kibanda chako mwenyewe taratibu usikubali mume ajue kikishakamilika andika hata jina la mwanao na pangisha ili siku mambo yakienda kombo usihangaike kuteseka sana.

  Hapo kwenye red mhh:A S 13:
   
 15. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hii sheria yako itakubackfire siku moja
   
 16. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kwa nini siri? wakati mwanaume anakuambia vitu vyote? jenga wakati anajua kama vyake anaandika majina yake tu na ya kwako andika jina lako maisha yanaendelea. haya mambo ya kujenga nyumba kumwandika mtoto mimi sifagili ndio utakuta mtoto anakuwa mjinga cause anajua mali zote mmemuandika yeye. akue atafute vyangu nitampa wakati ukifika
   
Loading...