Wanaume na makundi yao

Wanaume na makundi yao

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
912
Reaction score
3,006
Nimefanya tafiti japo siyo ramsi kwa kugawa wanaume katika mazingira matatu kwa kuzingatia aina ya malezi na makuzi yao, makundi yenyewe ni haya

1. Wanaume waliolelewa na mama tu katika utoto na ujana wao. Wengi wanapofika umri wa mtu mzima huwa na tabia hizi. Wengi ni wastaaraabu, hawapendi usumbufu na sio watu wa kujingiza kwenye tabia hataarishi. Hawa wengi huridhika sana na maisha yao hata kama kipato chao ni kidogo, mfano ukimkuta ni mwalimu huyu atashinda muda wote kazini, atawahi kurudi nyumbani akae na familia yake, hawezi engage kwenye tabia hatarishi, hawa anaweza pigwa na mke na asichukue hatua yoyote, wasafi wa mwili na mazingira.

2. Wanaume waliolelewa na baba tu. Wengi ni katili, watu wasiojali, always ni watu wa ku-risk maisha, pia sio wasafi wa mwili na mazingira. Ndio hawa ukimkagua anakolala unaweza panic, ila wengi ni watafutaji sana.

3. Wanaume waliolewa na wote. Hawa huwa hawaelewiki, na wengi tabia zao zinafana na kundi la pili tabia nyingine ngumu wanapenda sana ngono na pombe, ndio kundi la walevi wengi.
 
Waliolelewa na mama tu kuna tabia za kiume huwa wanakuwa hatarini kuzikosa kama mama sio jemedari na hajui maana ya kuwa na mtoto wa kiume.
Ni kweli wengi hawana vitabia vya kiume.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Tabia ya kundi la 3 wanakuaga nazo watu wa kundi la 1.
Hapana aisee nimewatazama rafiki zangu wengi, waliolewa na wazazi wote wawili na mimi nikiwemo, wengi ni watu wasiotabirika kabisa, kuna nyakati ni risk taker kuna nyakati huwa ni muoga, ila ndio wanaume wanaoshinda bar saa nne, walevi, uhuni uhuni flan nk
 
Waliolelewa na wajomba,
waliolelewa na bibi,
waliolelewa na babu,
waliolelewa na kaka,
waliolelewa na dada,
waliolelewa na binamu,
waliolelewa na mpwa,
waliolelewa na shemeji,
waliolelwa na mashangazi,
waliolelewa kwenye vituo vya yatima,
waliolelewa na majambazi,
waliolelewa na wachawi,
waliolelewa na mchungaji,
waliolelewa na padri,
waliolelewa na sheikh,
waliolelewa na wanachama wa CCM,
waliolelwa na CHADEMA,
waliolelewa na wanachama wa JF

listi ni refu sana tunaomba uendelee kutujuza
 
Waliolelewa na wajomba,
waliolelwa na mashangazi,
waliolelewa kwenye vituo vya yatima,
waliolelewa na majambazi,
waliolelewa na wachawi,
waliolelewa na wanachama wa CCM,
waliolelwa na CHADEMA,
waliolelewa na wanachama wa JF

listi ni refu sana tunaomba uendelee kutujuza
Hope na wewe unaweza kuwachunguza na kujua tabia zao, nimezingatia makundi ya walio wengi.
 
If i will get paid for that naweza fanya, lakini vitu kama hivi tuwachie watu wa physcology , sina sababu ya kutafta kuaminiwa ndugu
unaonaje ukafanya utafiti rasmi ili nikuamini zaidi
i
 
Mimi no no. 1 na umenielezea ukweli mtupu kasoro la mke akifanya kitu ya ujinga nimuangalie tu, hatoboi pia nina katabia kamoja umekaweka no. 3 mwisho mwisho ndo kananichanganya kalipotoka.
 
Utafiti wako umefanya kwa watu wangapi kwa kila kundi ,study case yako ilkuwa wapi na methodology gani ulitumia
 
1. Wanaume waliolelewa na mama tu katika utoto na ujana wao. Wengi wanapofika umri wa mtu mzima huwa na tabia hizi. Wengi ni wastaaraabu, hawapendi usumbufu na sio watu wa kujingiza kwenye tabia hataarishi. Hawa wengi huridhika sana na maisha yao hata kama kipato chao ni kidogo, mfano ukimkuta ni mwalimu huyu atashinda muda wote kazini, atawahi kurudi nyumbani akae na familia yake, hawezi engage kwenye tabia hatarishi, hawa anaweza pigwa na mke na asichukue hatua yoyote, wasafi wa mwili na mazingira.
"Nawaza kazi zangu tu, kinachonitesa sana ni wanangu kuwa siishi nao (ni kitu ambacho kinaniumiza sana) imefika wakati naweza toka shule ninapofundisha na kwenda kuwasalimia na huwa natoa hadi machozi nikifikiri why siishi nao, ila linapokuja suala la kuishi na mama yao inaKuwa mtihani, msaada wenu napokea ushauri , napokea pia matusi na kejeli, i'm old enough na maisha ya mtandaoni nayafahamu"
Moja ya maneno yako ktk uzi wako link hapo chini:
Sina hamu kabisa ya kuoa na umri unazidi kwenda
 
Back
Top Bottom