Cha ajabu wakati tungali tupo wapenzi,aliniaga kwamba anakwenda kwao kuwaona wazazi wake ,toka siku alipoanza safari hakupatikana kwenye simu ,baada ya wiki moja alilejea tena,na nilipomuuliza kulikoni mbona toka aondoke alikua hapatikani kwenye simu akanieleza simu yake ilikua mbovu,nilipomuomba anipe ili niipeleke kwa fundi akaniambia atanipa tukagombana sana na hakuweza kuleta ile simu,baadae niliamua kupuuzia na kumsamehe,nikamnunulia simu nyingine maisha yakaendelea,Kumbe inaonekana baada ya yeye kuondoka hakwenda kwao,akawa ameondoka na yule jibaba kisafari baada ya kuanza safari wakaanza kugombana na yule mzee akaamua kumnyang'anya simu kwa sababu wakati wakiwa njiani kuna mwanaume alimpigia na demu kashindwa kuongea kwavile yupo na mzee.