Correction: Kwanza kabisa, hakuna binadamu asiyekuwa na kasoro. Mungu pekee ndio mkamilifu asiyekuwa na kasoro.
Pili, si wanaume wote wenye tamaa, ambao hawaridhiki na walichonacho. Kama wewe uliamua kukurupuka na kuolewa na mtu usiyemfahamu vizuri tabia yake kwa shauku ya kutaka kutaka kuolewa, basi hilo ni kosa lako, hivyo usituingize sisi wengine tusiohusika kwenye hilo kundi.
Tatu mke mwema anayejiheshimu na kuheshimu ndoa yake, kamwe hawezi kuleta mambo ya ndoa kwenye mitandao. Ndoa ni kitu kitakatifu na chapaswa kuheshimiwa. Kama mna matatizo kwenye ndoa yenu, elezaneni na kuyatatua wenyewe. Ikishindikana mnaweza kupeleka kwa wazazi, wasimamizi wa ndoa, walezi au viongozi wa dini. Lakini wewe umekuwa ukifanya otherwise; wewe umekuwa ukianika siri za ndani ya ndoa yako tokea siku ya kwanza ulipoolewa. Sasa tukiangalia hapo kati ya wewe na yeye, ni nani mwenye kasoro? Toa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako, na hivyo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho katika jicho la mwenzi wako.