Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,349
Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.
Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.
Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.