Inakuwaje unaacha kunywa chai kwako unaenda kunywa chai hotelini ,unakunywa chai ya maziwa kwanini usinunue kwako maziwa mkeo akapika mkanywa na wanao,,,hujisikii vibaya wala kujishtukia au kujishuku?
Sio jambo jema kabisa,na sio haki yaan wanawake hebu kuweni wakali kabisa waume zenu muwabane wawe wanakunywa chai home kama ni ya rangi mnywe wote,,,halaf muwadai pesa za matumizi waongeze wenzenu wanatanua huko bar bill kubwa laki au zaidi we unakunywa chai ya rangi mnywe chai ya rangi kwa kupenda n mle vizuri
Wanaume na nyie acheni ubahili kama mnavyoonyesha ubavu na ujeuri wa pesa bar,tunawaomba na majumbani mwenu muanze hiyo jeuri muache matumizi ya kutosha watoto wale vizurii, sio watoto kula vizuri mpaka matumbo yanapata mshituko maana hayajazoea kula vyema
Pendeni familia zenu basi ,,wanasema family first
mkiwa bar utasema nyumbani pako vyema ,ukienda nyumbani hovyoo hovyo watoto wanakula kwa kulamba lamba tu hawashibi sio vizuri kabisa
Nadhani nimeeleweka na mjirekebishe mle hotelin kwa sababu maalumu alaa
Mkuu unayoyaongea yote haya ni kweli yanatokea kwenye familia nyingi sana.wakat mwingine sisi ndio chanzo au wakati mwingine ni wanaume.sina uzoefu sana ila nitajitahi kuchangia.
Marafiki zangu wengi sana ni wanaume sio wavulana hapa naimani umenielewa.nimekuwa nikiwauliza mara chache chache tunapokutana ni nini kinachwaboa mpka hawatulii nyumbni.huwa wanaongea vitu vinavyofana kila mmoja ninaekaa nae.
Anaanza na kutuponda sasa "hatukai nyumbn kwa kuwa mnakelele sana,mara housemaid kafanya hivi,mara hamjui kutupatia chakula tunachokipenda,ohooo hamko nadhifu,mara sijui nini"
Na mengine ni kuwa hawapendi kutoka na wake zao maana mda mwingi anautumia kununa,mara akipita msichana ukamwangalia kwa bahati mbaya imekuwa shida!nyumbani siku hiyo hakutakalika
Na pia hawapendi kutoka na wake zao kwa sababu unaeza ukakuta bei ya chakula hapo ni kubwa sasa shughuli ikija kwenye bill ikiwa kubwa eti madai yao tunaanza kulalamika wanatumia hela vibaya
Nyingine tena yani mambo ni mengi.eti kwa mfano mwanaume ni mpenzi wa movie akikaa kuangalia movie mkee anakuwa bubu au wakati mwingine anamtoa kwenye uwepo wa movie(hii ni kweli kabisa wengi wa wanawake tunahii kitu.yani unakuta kila kiungo kiko kinaangalia movie mtu anakujia mara ohoo vipi sasa ile ada ya mtoto!!jamni hii huwa inanikera hata mimi Chakorii)
Ya mwisho kwa leo ni kwamba....wakati mwingine wanataka kukutana na marafiki zao ili kubadilishana mawazo na kupeana michongo ya maisha.
************************************
Ngoja twende mbele turudi nyuma ni kweli kabisa wakati mwingine wanawake tunajisahau wakati mwingine jmni.huu ndio ukwel.
Lakini na ninyi wanaume si tuchuliane jmn mbna sote ni binadamu...hakuna mkamilifu wandg.tuchukuliane nawaomba.
Na sisi wanawake jamani tuwasome tu hawa wanaume wetu.jua ukimfanyia nini kwake ni udhaifu umemuwin.
Kama anapenda chakula kitamu mpikie,kama anapenda kilaji mnunulie (hapa inabidi umshtukize usimwambie kama utamnunulia kilaji maana anaweza kukupiga stop akasingizia hanywi kwa siku hiyo kumbe anataka akanywe huko bar kwenyewe.)
Tuwe tunadilikabadilika jamn.itatusaidia kuwa wapya kwa hiyo mijibaba.kama anakuhudumia vizur mamaaa hakuna namna inabidi ujitoe ufahamu kwa mumeo.
Na nyie wanaume sio mnapendwa huku halafu mnaenda kujitapa huko "mke wangu hapindui ananipenda mno"unaanza kumuumiza sasa..weee..
Mwanamke ukiwa mchakarikaji inaleta heshima ndani ya nyumba.hili ni muhimu.
[emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6] nimekula nini leo mbn naandika sana hivi kha!
Kamchango kangu hakooo...kama kunaambae atakwazika na hii comment yangu,tusameheane tu hakuna namna.
Wanawake tupunguze midomo.