Wanaume kuogopa wanawake

Wanaume kuogopa wanawake

Mnadharau sana ndio utasikia mwanaume suruali
Kuna dogo namfahamu alitupiwa virago nje..ila cha ajabu baada ya miezi minne karudi kule kule..
Unajua kuna wanaume wanajibweteka sana na hawawezi kuhangaika so wanaona huko ndo kwa kuponea..ila all in all ni maisha mabaya sana..imagine eti unakaa kwa mwanamke, kitanda chake, tv yake, sofa zake mpaka vijiko vya kwake..kweli kuna ndoa hapo?
 
Kuna dogo namfahamu alitupiwa virago nje..ila cha ajabu baada ya miezi minne karudi kule kule..
Unajua kuna wanaume wanajibweteka sana na hawawezi kuhangaika so wanaona huko ndo kwa kuponea..ila all in all ni maisha mabaya sana..imagine eti unakaa kwa mwanamke, kitanda chake, tv yake, sofa zake mpaka vijiko vya kwake..kweli kuna ndoa hapo?
Bonge la Aibu

Hiyo wanaume wa kaskazini hatuwezi aisee
 
Wanawake wanaojifanya wasomi na wenye hela ni pasua kichwa ,wana dharau balaa
 
Habari zenu sana jf

Kuna jambo linanitatiza hapa na sijajua if lina ukweli ndani yake au la. Siku ya X-mas nilikua na rafiki yangu mmoja tukawa tunapiga story, akaniambia kuwa ukiwa msichana, unafanya kazi, unajiweza, una gari inabidi uolewe.

Mimi nikamjibu kwamba ndoa sio jambo la kukurupuka, mpaka sasa sijaona atayenifaa na ambaye nitaendana nae. Sasa nilipomwambia kuolewa is not my priority nina plans zangu za maendeleo zaidi like kujenga nyumba etc alihamaki akaniambia,"Shosti wanaume watakuogopa na hutaolewa kamwe".

Hii statement imenishangaza. Kwahiyo eti nisifanye maendeleo yoyote eti sababu wanaume wataniogopa? Mbona wanawake tumekua watumwa wa ndoa hivi? Kwanini nisifanye kitu roho inapenda kwa kuhofia hiyo kitu?

Swali langu ni je ni kweli wanaume huogopa wanawake waliowazidi kipato? Kama ni kweli ni kwanini? Kwani mwanaume akinioa anashindwa kuja kuishi kwenye nyumba yangu?
Hata mimi siwezi kuoa wa hivyo bora nitafute wa la saba tu ...
Utanyanyasa sana
 
sio kuwaogopa, mwanaume anaogopa tabia zenu tu mkishapata Mali na kisomo.
jeuri .
na zaidi sana mwanamke wa hivi hutaka kumtawala huyo mwanaume na kumuamria mambo mengine.
kwa mfano marufuku ya muda wa kurudi nyumbani,kumchagulia marafiki, muda wote muwe pamoja,wivu juu, kumfokea mume mbele za Watu au hata watoto ukijua kuwa unamfuga,maneno ya kejeli kwamba unamhudumia kila kitu hajiwezi,mwisho kumpigisha kazi za ndani ukiwa kwenye sofa unaangalia TV.
unasahau maadili ya asili ya kiafrika,utii wa mwanamke wa kiafrica, suala la maji bafuni,chakula mezani,kitanda na hata nguo ya kuvaa kesho yake kwa kusoma kwako kwingi na Mali zako utavitakia haki Sawa au ufanyiwe wewe vyote hivyo.ukweli ni kwamba HAKUNA MWANAUME YEYOTE HATA AWE FUKARA VIPI ATAKAYE KUBALIANA NA UJINGA KAMA HUU NA NDO MAANA HUWA HAWAJI .
Nna binamu yangu mmoja juzi kati kaachwa hivihivi na watoto wawili kwa vitabia kama hivyo hapo juu.jamaa karudia maisha yake ya hali ya chini yenye Amani.
haifiki hata asilimia moja ya wanawake wenye kipato kikubwa ,elimu na maisha bora wenye uwezo wa kuelewa ofisini wawe bosi na nyumbani wake ni wake.
KAMA WEWE UNADHANI NI MMOJA WAO, GO AHEAD!!!ALL THE BEST
 
wanawake wa siku hizi pasua kichwa asilimia kubwa wao wanataka wanaume ambao wana kazi nzuli, mshahara safi, wana nyumba ,

wewe usiekuwa na kitu utaitwa mwanaume suruali
 
Hawaogopi wapo wanaume wengi wanawasomesha wake zao na wengine wanawapa mitaji, lakini wanawake wa Afrika ni malimbukeni wa mali akifanikiwa tu ndoa inakuwa chungu,. .Na jamii zetu pia bado zina ujinga zinataka zione mwanaume ndiyo mwenye kipato kikubwa kwenye ndoa kuliko mwanamke. Mwanamke mwenye kipato kikubwa kuliko mume wake anatakiwa amuombe Mungu ampe hekima sana, maana hata ndungu wa mke na marafiki hua hawapendi wanaona kama huyo mwanaume anafaidi,
 
Siyo kwamba wanaume wanaogopa wanawake walio vizuri kiuchumi ila kutokona na uzoefu na case tunazozijua huwafanya wanaume kutilia mashaka mustakabali wa mahusiano yenu ya mbele. Wanawake wengi (siyo wote) hushindwa kuheshimu waume zao pindi wanapokuwa na kipato kuwazidi. Hapa tatizo ndo huanzia ukizingatia kwamba hakuna kitu mwanaume anatamani kama heshima kutoka kwa mke wake. Ni kama amabavyo ninyi mmekuwa mkiomba kupata wanaume wanaojali na kuwabembeleza kwasababu hiyo ni asili yenu. Na heshima ni asili kwa wanaume karibia wote.

Mara nyingi wanawake waliotoka sana kimaisha hujikuta wanatokewa na wanaume ambao kwao shida yao ni mali ya huyo mwanamke. Kwahiyo hukibali lolote hata kama ni kudharauliwa ili mradi wapate wanachotaka lakini si kwamba huwa wameridhika kwenye roho zao. Ndio maana utakuta wanaume wa namna hii hutumia hizo mali za mwanamke kuhonga wanawake wengine ambao kwao hujisikia wanaheshimika kwa hao wapenzi wao.

Najua wanawake wengi watakuja juu kuhusu hili ila mi uzoefu wangu kwa ninaowajua wengi ni huu nilioueleza.
 
Hawaogopi wapo wanaume wengi wanawasomesha wake zao na wengine wanawapa mitaji, lakini wanawake wa Afrika ni malimbukeni wa mali akifanikiwa tu ndoa inakuwa chungu,. .Na jamii zetu pia bado zina ujinga zinataka zione mwanaume ndiyo mwenye kipato kikubwa kwenye ndoa kuliko mwanamke. Mwanamke mwenye kipato kikubwa kuliko mume wake anatakiwa amuombe Mungu ampe hekima sana, maana hata ndungu wa mke na marafiki hua hawapendi wanaona kama huyo mwanaume anafaidi,
Hii ni kweli. Ikitokea ukaoa mwanamke anayekuzidi kipato utasimangwa na ndugu zake. Mara nyingi wanakuwa na hisia kwamba umekwenda kumchuna ndugu yao.
 
Heshima ndio shida hapa na mambo ya kuitana mwanaume suruali.
 
Jinsi umeandika na simulizi yako tayari NISHAKUOGOPA.......KUNAKUOLEWA MWANAUME HAPO
Huku tunasema KUWEKWA KING'ASTI
 
Back
Top Bottom