Wanaume kuogopa wanawake

Wanaume kuogopa wanawake

Habari zenu sana jf

Kuna jambo linanitatiza hapa na sijajua if lina ukweli ndani yake au la. Siku ya X-mas nilikua na rafiki yangu mmoja tukawa tunapiga story, akaniambia kuwa ukiwa msichana, unafanya kazi, unajiweza, una gari inabidi uolewe.

Mimi nikamjibu kwamba ndoa sio jambo la kukurupuka, mpaka sasa sijaona atayenifaa na ambaye nitaendana nae. Sasa nilipomwambia kuolewa is not my priority nina plans zangu za maendeleo zaidi like kujenga nyumba etc alihamaki akaniambia,"Shosti wanaume watakuogopa na hutaolewa kamwe".

Hii statement imenishangaza. Kwahiyo eti nisifanye maendeleo yoyote eti sababu wanaume wataniogopa? Mbona wanawake tumekua watumwa wa ndoa hivi? Kwanini nisifanye kitu roho inapenda kwa kuhofia hiyo kitu?

Swali langu ni je ni kweli wanaume huogopa wanawake waliowazidi kipato? Kama ni kweli ni kwanini? Kwani mwanaume akinioa anashindwa kuja kuishi kwenye nyumba yangu?
Ndugu yangu fanya mambo yako ambayo wewe unaona Ni priority kwako. Kuna baadhi ya kina dada kuolewa sio priority kabisa Na huenda wewe Ni mmoja wapo. Fanya issue zako ambazo ww unaona ndio the best kwako. Ukweli Ni kwamba mwanaume yoyote ambaye yupo committed Ni Mara chache Sana Sana kuowa mwanamke ambaye tayari amesha jiestablish.
 
Ww dada sikiliza wanaume wanamuogopa demu hata akiwa na simu nzuri kuliko yeye, sembuse nyumba na gari?

wengi wa akina dada hawajaolewa kwasbb tu walijieleza kwa wachumba zao kuwa wana viwanja (plots). uchumba ukakomea hapo.

ukificha ukaja ukasema baadaye ndo kabisaaa, balaa lake ni kubwa.

KWANINI WANAOGOPA?
imeandikwa "Enyi wanawake watiini waume zenu nanyi wanaume wapendeni wake zenu". sasa unajua maana ya kutii dada? ni kama vile jeshini, hakuna kuhoji na hakuna demokrasia. utayafanya haya wakati nyumba na gari ni vyako? si utaropoka?

lkn pia imeandikwa mwanamke atawaacha baba na mama yake aende kwa mume. kinyume chake hapana.

Kwahiyo Ni Maagizo Toka Juu Mbinguni.
 
Alichokuambia rfk yko kpo sahh kbsa hajkosea tena km una mpngo wa kuolewa mshukuru kw ushaur wanaume hawapend kunyanyask sbb mke anakpto kikubwa mana tunawajua nyie mkifanikiwa sasa ple hm ww ndo utakuwa na saut nan akbl hyo km ueongo jrb utaishia kumlk watoto co mume
 
Mimi ni mmojawapo! Mwanamke akiwa kapuku tu Anadharau,je akiwa hivyo si balaaa...Huo ndio ukweli.Sitakubali maisha yangu yote...
 
Sijawahi ogopa mwanamke,hata kama
nitapata nafasi ya kukaa meza moja na Angeline Jollie nitamtongoza!
Mwanamme anayeogopa mwanamke kwa sababu ya vihela vyake ni mwanamme wa Dar'
 
Ni nadra sana kuolewa. By the way fanya maendeleo yako usiogope, zari the boss lady ana mkwaja wa maana, majumba na magari na anazalishwa kila uchao maisha yanasonga
 
Fanya utafiti wanaume wasio na vipato wananyanyasika sana ndoani ...hawana say yeyote hata mbele ya watoto!
 
rectify ur statement madam.... cjawa kumuona kuona mwanaume akiogopa binafc ila i know the fact kwamba hawatakii... coz hao wanawake wana mashauzi kidgo tu mkikorofishana mtu unakimbizwa and ni udhaifu mwanamke kusimamia mahtaji ya familia wakat mwanaume una nguvu za kutosha and uko tu hom
 
kila mmoja afanye tafiti kwa wakati wake...
ni kiasi gani wanawake wabunge wapo single mama au wale wenye nyadhifa kubwakubwa za kitaifa....??... au wanawake wenye uchumi mkubwa....
hizo asilimia ndio majibu ya uzi wako......
 
Back
Top Bottom