Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,377
- 3,394
Unaweza kukuta kipaji pekee alicho nacho ni hiki cha kunengua.
Nimekuwa nikijiuliza siku nyingi sana kwamba, wanaume wanawachukuliaje mabinti wanaocheza shoo maarufu kama madansa? Naamini kabisa kwamba mtu kuwa mcheza shoo au dansa ni kipaji kama ilivyo vipaji vingine. lakini kwa bahati mbaya sana kuna nadharia imejengeka miongoni mwa jamii kwamba, mabinti wanaocheza shoo au madansa ni malaya na imani hii imejikita vichwani mwa wanaume wengi.
Unaweza kukuta binti mzuri anayejiheshimu na kipaji pekee alicho nacho ni cha kucheza shoo au dansa. Kipaji hicho ndicho kinachomuwezesha kujikimu katika maisha yake na kujiletea maendeleo. Ni shughuli ambayo amekuwa akiifanya kwa muda mrefu, lakini kwa bahati mbaya kila mwanaume anayemtokea anapokuja kugundua kwamba shughuli anayoifanya ni ya kucheza shoo au u-dansa anaingia mitini.
Maswali yangu kwa wanaume ni haya:
1. Je unaweza kum-DATE au kumuoa mwanamke ambaye ni dansa au mcheza shoo?
2. Kama itatokea umempenda na ungependa awe mke wa maisha yako, Je utakuwa tayari kumuacha aendelee na kazi yake ya kucheza shoo au utamkataza?
CC: Mentor, Kiranga, Nyani Ngabu, Kaizer, Asprin, Mr Rocky, Erickb52, Arushaone, PakaJimmy, Nicas Mtei, Jiwe Linaloishi, jouneGwalu, Vin Diesel, Kipaji Halisi, KakaKiiza, mayenga, ayanda, Mwita Maranya, The Boss