Wanaume hudhurieni leba pindi wake zenu wanapojifungua

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Wizara ya Afya imekuwa ikiwataka wanaume kuhudhuria leba pindi wake zao wakijifungua ili kusaidiana na mama mzazi katika majukumu tofauti ikiwemo kuhakikisha mtoto ni wa mzazi sahihi.

Kufuata vifaa ama bidhaa dukani kwa ajili ya mama mzazi, kumshika bega mama mzazi pale anaposhindwa kutembea nakadhalika.

Ikumbukwe hapo awali, wanaume walitafsiri kitendo cha kuhudhuria leba kama aibu pasipokujua kuwa mama mzazi anapokuwa mwenyewe wakati wa kujifungu, kunaweza kuwa na hitilafu mbalimbali ambazo kama baba mzazi angekuwepo basi zisingetokea.
 
Mwanaume ukienda huko utashangaa hao manesi wenyewe ndo wanakuwa wa kwanza kukushangaa imekuwaje upo apo. Hapo Manesi ndo wafundishwe kwanza kubadili mtazamo wao kwa wababa wanaoenda na wake zao hospitali
 
Pa1 na dunia kubadilika kimtazamo juu ya mambo mengi likiwemo hili la kwenda clinic, tunakokwenda sijui kwa kweli kama tutatofautisha mwanaume na mwanamke kimajukumu

Niseme tu asante hayo hayakunikuta enzi hizo!
 
Back
Top Bottom