Wanaume hili sio la kuvumilia, kimbia mbio

Wanaume hili sio la kuvumilia, kimbia mbio

Meizon

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
279
Reaction score
105
Heshima kwenu MMU,

CAUTION;

Imefanyiwa utafiti kwamba a woman can speak 50,000 words per day wakati a man speaks only 5,000 per day. Hiyo ni ukitaka kulinganisha. Guys kama unataka kufa kwa matatizo kama stress,Bp gombana na mwanamke, they talk too much nifafanue.

Mwanaume ukikasirika sana mwili una secrete massive amount of Cholesterols kama lubricant ili kukaa tayari kupigana, sasa mnapoishia kugombana afu no fighting yale mafuta yana kosa kazi afu kadri mnavyozidi kulumbana basi yanagandia kwenye mishipa ya damu, matokeo yake Blood pressure inaongezeka afu baadae kifo! Ndio maana siku hizi wanaume tunakufa katika umri mdogo hii ni moja ya sababu.

Mume akitoka kazini kashatumia maneno 4999 anafika home badala ya kubembelezwa na kupumzishwa anaanzishiwa dialogue kali. Blah blah blah aagrr hasira hizo! Kama una mpenzi anakuweka kwenye hatari hii jamaa yangu run away, she will kill you. Huwezi kumshinda mwanamke kuongea!

Kwa wanawake waelewa, hili ni somo kwenu. Sisi wanaume Mungu katuumba hivi- we are one minded! Yani ubongo wetu unalenga direction moja, kama tunaangalia mpira basi jua mume wako anaangalia mpira coz akili yake yote iko pale! Ila wanawake daah!

Wanaweza fanya mambo 6 kwa mpigo, huku anapika, huku ananyonyesha, hapo hapo anaongea na simu na anapanga bajet ya kesho! Sasa ukielewa hivi hutamuua mwanaume wako kwa stress, sio anaangalia mpira wewe unaanzisha Baby hujaona nilivyosuka? Mbona hunisifii? Lazima mgombane kwasababu unamvuruga tu, hasa kama anafungwa.

Nimeamua kuandika hii thread baada ya kumsikia mama flani akiwasimulia mashoga zake eti mume wake kamshikisha adabu! Yani jamaa hawezi kuongea kabisa, afu kaoa vuvuzela moja amazing. Kila siku anapigiwa kelele hadi mtaa mzima wanakusanyika kusikiliza!

Jamaa akisahau kutekeleza jambo dogo tu ni kelele hadi anaomba msamaha. Hasira zimemshika, kumpiga hataki,akikimbia ni mke wake yule kwahiyo atarudi tuu! Yani mwanamke ni ana maneno ya taarabu yanauma acha kabisa!

Afu yeye anajisikia raha kumcharukia mme wake, eti anamchamba!Nikasema acha niwasilishe JF ili kama wapo wanawake wa hivi humu mjue kuwa mnamuuwa baba watoto na kwa wanaume kama habadiliki okoa maisha yako!

Kimbia aisee, utakufa!
 
hahhahah yaah it's true en asante maneno kuntu kiukweli mda mwingine huwa wanawake wanakosea maana hujui mtu ana mood gani unakuja juu kama moto wa kifuu
 
Ni ngumu kuvumilia kuishi na mwanamke Mwenye makerere
 
They talk damn muuuuch....

Nataman kungekuwa na “mute“ remote ili akiianza tu kuropoka una mmute......
 
Yaani ni ukweli mtupu. Kuna siku wife ile anaingia ndani hata hajakaa wala hatujamaliza kusalimiana, akaanza kuniuliza mbona hujaniambia kama nimependeza kisa katoka kusuka nywele.
 
Kimbia fasta toka nduki we kimbia...
Ukianguka ukiumia inuka vumilia...

Ukiona vicheche vinakumendea kimbiaa...

Usije ukapewa kesi ya Babu Seya kimbiaa...

Maana hata virusi watakuletea...

Ni bora kukimbia kabla mambo hayajatokea kimbiaa...
 
Yaani ni ukweli mtupu. Kuna siku wife ile anaingia ndani hata hajakaa wala hatujamaliza kusalimiana, akaanza kuniuliza mbona hujaniambia kama nimependeza kisa katoka kusuka nywele.

Na ww ukamjibuje
 
ila kuna mianaume ambayo ikifika tu ndani inatafuta la kuongea sasa hawa ni wanawake au
 
Dawa ni kuvaa ma-earphone afu unaweka volume mpaka mwisho unasikiliza wimbo wa "uniguse tena" "unigusee" "ninaomba bwana uniguseee"
 
Hakuna kosa hapo kwa kuwa na yeye ndivyo alivyoumbwa. Utofauti huu ndiyo unaokamilisha maumbile. Huwezi kusema mwanamke anakosea kuwa na papuchi na mume anakosea kuwa na dushelele. Kinachotakiwa kujua kuishi pamoja pamoja na tofauti zetu huku tukicukuliana kwa upendo.
hahhahah yaah it's true en asante maneno kuntu kiukweli mda mwingine huwa wanawake wanakosea maana hujui mtu ana mood gani unakuja juu kama moto wa kifuu
 
Back
Top Bottom