Wanaume hii tabia ya 'kudanga' kama wanawake mnaitoa wapi?

Wanaume hii tabia ya 'kudanga' kama wanawake mnaitoa wapi?

Muzine

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2017
Posts
32,366
Reaction score
60,492
Habari wana JF?

Tunaunza mwaka vizuri lakini upande wa wanaume naona mmekuja na staili mpya ya kudanga kwa ajili ya kupata kitonga cha maisha.

Hii tabia ya mwanaume kuvizia wamama na wadada wenye pesaa ili muwatongoze na kuwalaghai mnaitoa wapi?

Ninachojua mm wadada ndio wana tabia hiyo ya kudanga kwa Masponsor. Kwahiyo huu Mmaka wanaume na nyinyi mnatafuta Masponsor kama dada zenu wanavyofanya.

Yani wanaume mnakaa kabisa kijiweni kujadili jinsi ya kumdangia mheshimiwa fulani mwanamke kweli vyuma bado vimekaza naona grease haijafanya kazi.

Zamani ukisikia kuna vikao vya Bunge Dodoma utaona wadada wanatoka Dar na mikoani kuja kuwadangia waheshimiwa lakin saivi imekuwa kinyume wanaume ndo wanadanga ili kupata pesa.

Badala ya kuitwa viben 10 mtaitwa viben 5 nawaambia.

Kumbe huwa mnatamani mambo ya kike, naona siku nyingi mlitamani kudanga sasa kutuita wadada tunapenda pesa ndo nini? Wakati na nyinyi mmekuja humo humo tu kwenye kudanga Masponsor.

Mwaka 2018 wanaume hatutaacha kuwaita viben 10 na mjiandae kuchezea makofi (in shilole voice)
 
Back
Top Bottom