Tabia hii ya wanawake/wanaume kupondana, je hamuaminiani?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,636
22,265
Hamjambo wadau,

Nimepitia mahusiano kadhaa ya kuwa na wanawake tofauti katika harakati za ujana, ila kuna haka katabia unakuta mwanamke wako anakutambulisha rafiki yake vizuri,lakini cha ajabu huyo rafiki yake akiwa na muonekano mzuri tegemea baadaye atakwambia;"umemuona yule rafiki yangu ni malaaya alikuwa na mwanajeshi baadae akawa na flani flani, amewahi toa mimba kadhaa yani hata hafai,alipopanga wanaume nyumba nzima katembea nao, kwanza sijui hapo kama ni mzima; n.k

Naomba kuwauliza wanawake hayo maneno ya kupondana huwa yana lengo gani? Kwanini umpondea na kumpakazia ili mradi tu hadi aonekane hafai hivi huwa ni kwanini? Hata kwa baadhi ya wanaume pia hii tabia ya kupondana huwa naiona, unakuta unamtambulisha rafiki yako vizuri kwa mpenzi wako halafu baadaye,''unajua yule rafiki yangu ni mlevi, ametembea na mabamedi bar zote anajulikana, mda wote viroba halafu hiyo gari aliyonaye si yake'' n.k

Naomba tuambizane ukweli hapa lengo kuu huwa ni nini? JE HUWA INASAIDIA NINI UKIMPONDA RAFIKI YAKO KWA MPENZI WAKO?
 
Sasa mkuu wewe umeshindwa kuwaambia wanawake wako halafu unakuja kuwalalamikia hapa ili iweje? Au na wewe ndo wale wale?
 
Back
Top Bottom