angelita
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 3,017
- 2,445
Leo nije kwakina kaka. Kwakweli sikufahamu kuwa hadi miaka ya dot.com bado watu wanakataa ujauzito na watoto, really?
Wakati unafanya hilo tendo na huyo dada hukujua kuwa matokeo yanaweza kuwa nini? Wako wapi vijana wanaojua thamani ya msichana na kumsubiri hadi siku ya harusi? Wako wapi vijana wanaosimamia na kuamini wanayoyasema?
Vijana wa siku hizi wamejaa mashairi mazuri mno ya mapenzi, yaani maneno yao yanawamaliza kabisa wadada hata wakilokole wanajikuta wametoa yote. Inapotokea mimba basi huruka mita mia, kama sio yeye kabisa, mashairi ya kubembeleza yanageuka mikuki ya kuchoma moyo.
Umeshamkosea Mungu, Dada amepata mimba nijukumu lako kuutambua ujauzito huo na kuulea pamoja na mtoto. Wengine wanawashauri wasichana watoe mimba, na wasichana kwakutokujua lakufanya wanakubali. Nijambo la aibu Sana kukataa mimba na mtoto wako, na akishafika miaka 5 unajitutumua Mahakamani kumdai mtoto, mbaya Sana.
Wewe kijana unayesoma hapa, Mungu anajua ni watoto wangapi umewakataa. Tubu sasa mbele za Mungu na haraka uende ukaombe radhi kwa mama watoto wako na ukubali majukumu yako.
Source: www.rosemarymazizi.blogspot.com