Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
Ukiachilia mbali uzuri wa mtu, tabia yake, utanashati na mengine mengi, kila mwanaume ana ladha anayoitafuta kwa mwanamke anayemtaka. Hii inatofautiana kati ya mtu na mtu, siwezi kuongelea nini mwanaume anatafuta kwa mwanamke, ila najua kuna aina Fulani za wanawake wanaume wengi hawapendi kuwa nao.
Waongeaji Sana
Wanawake wa maneno mengi, wanaume hawapendi mwanamke mropokaji. Wanawake wa aina hii huwa hawajui nini waongee na nini wasiongee au wakati gani wa kuongea na wakati gani wa kunyamaza. Watu wa aina hii hawajui kuuliza, wao wanafoka tu mwanzo mwisho.