Wanaume Andikeni "Wosia" mapema

Wanaume Andikeni "Wosia" mapema

Naomba kuuliza, kwani mme au mke akifariki pasipokuwa na wosia, ni nani anayestahili kurithi mali? Kwani hakuna sheria ya mirathi inayo-define warithi wa mali?

Ukifika bila wosia, Kikao cha ukoo kitaitishwa na kumchagua msimamizi wa mirathi ambaye atashirikiana na wanaukoo wengine kugawa mali.
 
Tatizo la kutoandika wosia kwa jamii nyingi za waafrika hasa watanzania ni kutokana na Mila na Imani potofu kuwa unakuwa unajiletea uchuro na mikosi ya kifo kukunyemelea.
 
Je sharia za nchi zinasema nini kuhusu mirathi ? Nimewahi kuona wandugu kuja na kuchukua kila kitu na kuacha kidogo kwa watoto na mama yao kwa madai hiyo ndio mila yao. Waslam wana sharia zao za urithi na ni dhahiri nani anastahili na kiasi gani.
 
Urithi ni haki ya Mtu kinachokuja Kuchanganya ni Magawanyo Yenyewe ...hasa Wosia usipokuwepo..

Nashangaa Watu wanavyosema Tafuteni Vya Kwenu.. Mtu unakuta Unakila Kitu na Una Kwako ila Mzazi anapofariki Umeandikwa Pia kwenye Urithi sasa Uuache kisa Una kila Kitu.. Inabidi utumie hekima Kuuagawa au Kuutumia huo Urithi.. na Uendeleze ukoo

Watu Hamuoni Makapuni makubwa Ya Nje yanayomilikiwa na Familia Toka Miaka ya 18 huko yanaendaje...mpaka Leo yapo...

Acheni hizo bhana...
 
Ila ukifa ujue ushamaliza kazi yako hapa dunian na kimsingi huwezi tengenezea mtu yeyote maisha hapa dunian ili eti ukifa asiteseke.....Hakuna jema hata moja achia watoto urithi wa mali ukifa tu wanauza mali zote nadhan mifano ipo kibao....Wachia urithi mke wako baada ya wewe kufa atakutana na Manuu hapa nitamchanganya tutakula mali zako zote nkishamailiza namtema.....So take it easy na we ukifa umekufa tu kwan yanaoendelea mara baada ya vifo laiti marehemu wangepata wasaa wakufufuka walau dk 1 waone mali walizoacha zinavyotobolewa angekufa kwa mara ingine.

Mkuu ni kweli marehemu wangekuwa wanafufuka wangeomba Mungu wafe tena haraka, mfano, Arusha kulikuwa na mzungu anaitwa bwana mila alikuwa na bonge la shamba, akazaa mtoto mmoja na mwanamke wa kiarusha, hakutaka mwanae apate tabu akamnunulia huyo sehemu nyingine nyingine akamjengea, mwanae alipokuwa akamchukua mama nae akaendelea kuzaa na wabongo, mzungu alipoona amezeeka akauza sehemu ya shamba akamuwekea mwanae hela kwenye A/c, akaacha sehemu ya shamba, kufa kijana akaanza kucheza kamari tena Nairobi hela ikaisha akauza baadhi yanyumba mwisho kauza shamba lote hela ikaisha akauza nyumba aliyokuwa anaishi amabapo mbele yake kuna kaburi la baba ake, akaja na watu wafukue kaburi la mwenye nyumba mpya akmwambia muache mzee apumzike. Huyo kijana kahama mji akiwa maskini kabisa. Yule mzungu alikuwa anampenda mwanae vibaya mno lakini mwanae shiiiida.
 
Sioni tatizo la mke au mume kutumia mali za marehemu na mke/mumempya...aliyekufa kafa bana...

Ukianza kufikiria nikifa mke wangu ataolewa tena afu akiolewa mume mpya atakula jasho langu baaasss...umekaribisha complications nyumbani kwako...

Back to the topic...wajita na wakerewe ni watata sana kwenye mirathi...kama umeolewa na haya makabila take care...najua kesi lukuki...tena ni mbaya hii cha mtoto...

Kuna watu wamekufa na hawajaacha hata mirathi lakini mambo yanakuwa shwari tu sababu ndugu wa mume wana roho za kitajiri...na si culture yao ku bank kwenye mali za marehemu...lakini hayo makabila pamoja na wajaluo...hacha kabisa....

Swala la urithi ni kweli arithi baba au mama je ni vyema baba arithi mali ya mkewe alefu atumie kwa wanawake wengine au mama alithi mali ya mmewe atumie kwa wanaume wengine watoto warithi mali ya MZAZI wao MZAZI atunzwe na watoto wake kosa hapo watoto hawatunzi MZAZI wao wapumbavu
 
Mi naona kuwafundisha watoto watafute vyao ni bora na hizo nyumba zibaki kuwa za familia nzima, msimamizi awekwe kati ya hao wanafamilia, nyumba isiuzwe
 
kuna watu wana tamaa yani mtu mzima unabanana kwenye urithi na mama mzazi duuuh!!!!
 
Waha wa Kigoma hawana shida na mirathi wala mtu akifa hamna anayefuatitilia mirathi. Wanaobaki mtajijua wenyewe
 
Jipange mnapokua hai kutegemea milasi ni kudumaza akili na kutafuta migogoro isio na sababu.

Watu wanatimba mahakamani kupapalikia milasi ata kaburi wanasahau kulimia loh! Binadamu sisi mungu atusaidie!.

Aturehemu kwa kweli ni kutojitambua
 
Kuna Kisa kimoja nataka niwashirikishe.

Mkabala na Nyumba niliyohamia hivi karibuni baba mwenye nyumba alifariki dunia, baba huyu aliacha mke na watoto kadhaa, aliacha na mali zikiwemo Nyumba, sasa huyu baba ni mjita na mke wake ni mkerewe, Mama huyu baada ya mume kufariki ndugu walikuja na kugawa urithi kwa "watoto", wa marehemu, mama yao akapewa chumba kimoja tu, na watoto wakapewa chumba kimoja kimoja katika nyumba hyo, Nyumba ina vyumba 6, kila mtoto alipewa chumba kimoja na mama yao akapewa chumba kimoja, sasa watoto wamishaoa, na kuolewa lakini vyumba vyao wamepangisha wapangaji, na pesa zinazopatikana kwa kupangisha mama yao anawatumia huko walipo, Sasa unakuta kwa mfano nyumba au choo/bafu linahitaji ukarabati, pesa za kufanyia ukarabati hakuna, mama yao anaishi maisha ya shida, na anasema kuwa hizo ndo mila za wajita!! ebo.

Hivi kuna aja gani ya kugawa urithi kwa watoto wakati mzazi mmoja bado yu hai?

Vijana ambao hadi tunaoa bado tunang'ang'ania urithi wa wazazi wetu ni sahihi?

Kwa nini wanaume hata wanawake tusiandae wosia mapema hata wa mdomo tu?

tabia zingine ni shidaaah. Na hata hao watoto ni vichwa maji
 
Urithi ni wa watoto na mzazi anayebaki awe msimamizi tu.
 
Urithi ni wa watoto na mzazi anayebaki awe msimamizi tu.

Unaweza ukawa sahihi au usiwe sahihi kutegemea na sheria ipi unayo refer...

Kama sheria ya serikali (si kimila, wala Kiislamu) ya ndoa mali ni za baba na mama na watoto wako nje ya picha...iweje mmoja akifa mali ziwe za watoto na mzazi alobaki awe msimamizi tu????

Na ukumbuke kuwa si wanawake wote ni magolikipa...maana hapa naona umemlenga mama...

Au sema mama kafa kabaki baba...basi huyu baba ghafla anakuwa muhudumu sijui mlinzi tu wa mali za watoto...hell no...

Watoto watatunzwa wakifika umri wa kujitegemea wasepe with or without kitu....

Najua abc za sheria za ndoa kwani nimeshuhudia ndoa inavunjika na watu wanagawana mali pasu kwa pasu...na mahakama wala haikutaja watoto....

Labda unambie nusu ya mali inaenda kwa watoto, nusu kwa mama au baba in case wameamua kugawana mahakamani...lakini mama ana mgao mkubwa zaidi ya watoto kisheria ya serikali (common law)
 
Kuna Kisa kimoja
nataka niwashirikishe.

Mkabala na Nyumba niliyohamia hivi karibuni baba mwenye nyumba alifariki
dunia, baba huyu aliacha mke na watoto kadhaa, aliacha na mali zikiwemo
Nyumba, sasa huyu baba ni mjita na mke wake ni mkerewe, Mama huyu baada
ya mume kufariki ndugu walikuja na kugawa urithi kwa "watoto", wa
marehemu, mama yao akapewa chumba kimoja tu, na watoto wakapewa chumba
kimoja kimoja katika nyumba hyo, Nyumba ina vyumba 6, kila mtoto alipewa
chumba kimoja na mama yao akapewa chumba kimoja, sasa watoto wamishaoa,
na kuolewa lakini vyumba vyao wamepangisha wapangaji, na pesa
zinazopatikana kwa kupangisha mama yao anawatumia huko walipo, Sasa
unakuta kwa mfano nyumba au choo/bafu linahitaji ukarabati, pesa za
kufanyia ukarabati hakuna, mama yao anaishi maisha ya shida, na anasema
kuwa hizo ndo mila za wajita!! ebo.

Hivi kuna aja gani ya kugawa urithi kwa watoto wakati mzazi mmoja bado
yu hai?

Vijana ambao hadi tunaoa bado tunang'ang'ania urithi wa wazazi wetu ni
sahihi?

Kwa nini wanaume hata wanawake tusiandae wosia mapema hata wa mdomo
tu?

its true the will will speak upon yo death " mr kahichile's words"
 
Kuna Kisa kimoja nataka niwashirikishe.

Mkabala na Nyumba niliyohamia hivi karibuni baba mwenye nyumba alifariki dunia, baba huyu aliacha mke na watoto kadhaa, aliacha na mali zikiwemo Nyumba, sasa huyu baba ni mjita na mke wake ni mkerewe, Mama huyu baada ya mume kufariki ndugu walikuja na kugawa urithi kwa "watoto", wa marehemu, mama yao akapewa chumba kimoja tu, na watoto wakapewa chumba kimoja kimoja katika nyumba hyo, Nyumba ina vyumba 6, kila mtoto alipewa chumba kimoja na mama yao akapewa chumba kimoja, sasa watoto wamishaoa, na kuolewa lakini vyumba vyao wamepangisha wapangaji, na pesa zinazopatikana kwa kupangisha mama yao anawatumia huko walipo, Sasa unakuta kwa mfano nyumba au choo/bafu linahitaji ukarabati, pesa za kufanyia ukarabati hakuna, mama yao anaishi maisha ya shida, na anasema kuwa hizo ndo mila za wajita!! ebo.

Hivi kuna aja gani ya kugawa urithi kwa watoto wakati mzazi mmoja bado yu hai?

Vijana ambao hadi tunaoa bado tunang'ang'ania urithi wa wazazi wetu ni sahihi?

Kwa nini wanaume hata wanawake tusiandae wosia mapema hata wa mdomo tu?

Kwa ndugu wenye ustaarabu na walio elimika; hii nyumba ingelibaki mikonni mwa familiya nzima ya marehemu (mke na watoto wake) mama akiwa ni msmamizi mkubwa kushirikiana na mtoto wa kwanza.

Mama aishi katika hiyo nyumba hadi mwisho wa maisha yake naye. na kama kupangisha baadhi ya vyumba inapaswa iwe ni kwa ajili ya kumsaidia mama matumizi yake.

Watoto wajitegemee na siyo kuishi kunywa pombe eti kutegemea baba ana nyumba kubwa na mali nyingi.

UPUMBAVu MTUPU!!!!!!!!!

Mzazi mmoja akiwa hai hiyo mali yake usitegemee mali ya Urithi. ni kuukaribisha umaskini.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Wosia ni kitu ya muhimu sana;
Na kwanini umesema wanaume; hata wanawake wana mali pia, au haujui?
 
Wosia ni kitu ya muhimu sana;
Na kwanini umesema wanaume; hata wanawake wana mali pia, au haujui?
Mali za mwanamke kama mume yupo hakuna shemeji anayeweza kuja kuleta kibesi. Ndo maana huwezi sikia migogoro ya aina hiyo. Labda siku za mbeleni maana life limebadilika hivi majuzi tu.
 
Kuna Kisa kimoja nataka niwashirikishe.

Mkabala na Nyumba niliyohamia hivi karibuni baba mwenye nyumba alifariki dunia, baba huyu aliacha mke na watoto kadhaa, aliacha na mali zikiwemo Nyumba, sasa huyu baba ni mjita na mke wake ni mkerewe, Mama huyu baada ya mume kufariki ndugu walikuja na kugawa urithi kwa "watoto", wa marehemu, mama yao akapewa chumba kimoja tu, na watoto wakapewa chumba kimoja kimoja katika nyumba hyo, Nyumba ina vyumba 6, kila mtoto alipewa chumba kimoja na mama yao akapewa chumba kimoja, sasa watoto wamishaoa, na kuolewa lakini vyumba vyao wamepangisha wapangaji, na pesa zinazopatikana kwa kupangisha mama yao anawatumia huko walipo, Sasa unakuta kwa mfano nyumba au choo/bafu linahitaji ukarabati, pesa za kufanyia ukarabati hakuna, mama yao anaishi maisha ya shida, na anasema kuwa hizo ndo mila za wajita!! ebo.

Hivi kuna aja gani ya kugawa urithi kwa watoto wakati mzazi mmoja bado yu hai?

Vijana ambao hadi tunaoa bado tunang'ang'ania urithi wa wazazi wetu ni sahihi?

Kwa nini wanaume hata wanawake tusiandae wosia mapema hata wa mdomo tu?

Katika hili naona ndugu hawakufanya makosa, as long as waliwagawia wana famili. Pili inategemeana na malezi ya familia. Katika familia zenye malezi bora na zenye upendo chamtoto ni cha mama na cha mama ni cha mtoto. I mean kama watoto wana uwezo na mama yao anashida wangeweza kumwachia hata kodi yote akachukua mama yao.

Ninachikiona hawa watoto nao ni choka mbaya. Hivyo kodi ya chumba kimoja nayo wanaitolea macho. If this is the case hata kama mama yao angepewa nyumba yote kusingekuwa na amani wange mzonga zonga tu.

Nimeona katika familia kadhaa kama watotio wengine wana uwezo mali kidogo za urithi wana waachie wale wasio na uwezo.

Kitu muhimu ni kuwawezesha watoto kujipatia mali zao ukiwa hai. Hawatasumbuka na urithi.
 
Back
Top Bottom