Wanaume Andikeni "Wosia" mapema

Wanaume Andikeni "Wosia" mapema

Naona kama na sie wanawake tuwe busy kutafuta

Hivi mali zetu tuweke majina yetu kama ikitokea mme ametangulia viwepo vyenye majina yetu??? au yelewiiiii
 
Mali za mwanamke kama mume yupo hakuna shemeji anayeweza kuja kuleta kibesi. Ndo maana huwezi sikia migogoro ya aina hiyo. Labda siku za mbeleni maana life limebadilika hivi majuzi tu.

Dunia imevaa bukta...kuna case moja nilishuhudia mama mmoja alikufa kwa kansa...sasa aliwai kwenda kutibiwa nje ya nchi akarudi na gari...miaka ile gari ilikuwa kitu cha maana sana...huyu mama alipona...baadae akaaugua sana akafa...

Ndugu zake walikuja kumnyang'anya mume wake gari...yani kila mtu alisikitika...ni wakerewe hao....na huyu mama si kwamba hakuzaa aliacha watoto wawili...acha kabisa....

Naona yule mzee hakuona sababu ya kupelekana mahakamani...au ndio mila zao...hata sijui...
 
Msaada: Format ya wosia pleese!

Mimi ---------------Endapo nitatangulia mbele ya haki nitataka Mali zangu zifuatazo zigawanywe kama nitakavyoelekeza hapa chini na Wosia huu ni sharti ufuatwe na kila mmoja kama unavyoshuhudiwa hapa.

Mali zangu ni........Nyumba 4, moja ipo .........ya pili ipo........ya tatu ipo...............na ya nne ipo....................

Gari 2, viwanja 3 cha kwanza kipo..................cha pili kipo.......................cha tatu kipo.............................

Na mgawanyo utakuwa kama ifuatavyo.........

Jumla ya watoto wangu wote wa kuzaa ni 3 wawili ndani ya ndoa na mmoja nje ya ndoa, Majina yao ni Bituro onduku, katikila onduku, na kate onduku.

Nina mke mmoja wa ndoa naye ni....................

Mgawanyo wa Mali zangu ni kama ifuatavyo:-

...................................;........................................;...........................................;
 
Back
Top Bottom