Wanatupanga ama ni kweli pameanza kuchangamka?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,388
Hii inaweza kuwa wiki ya kipekee kwa minong'ono mingi na ya kila aina huku "zile habari za chini ya zulia zikiwa nyingi"
Mengi yaliyotokea wiki Hi yana hisia mchanganyiko, uzushi halisi na maigizo..
1. Minong'ono kwamba kapteni Tesha yuko hai salama na huru nje ya nchi akiendeleza harakati

2. Habari za kuibuka kwa mkuu wa majeshi na kutoa onyo kwamba UTEKAJI SASA BASI LA SIVYO....! (Nimeona hii kama imekanushwa jana huko mitandaoni)

3. Kutekwa na kuuawa kwa mkazi mmoja wa Arusha mwenye sintohamu nyingi.. Utekaji huu ni kama vile ulikuwa jibu kwa mkuu wa majeshi aliyesema UTEKAJI sasa basi!

4. Kusambaa kwa habari kwamba mwafwere yamemkuta ya kumkuta

5. Kuibuka kwa kanali Augustine Polepole na kuendelea kutoa ultimatum mdogo wake aachiwe huru haraka pamoja na watu we engine akimtaja na Mdude pia
Kanali naye kampa Pole Mwafwere

6. Habari nyingi za TFF NA TMF.. makundi yanayosemekana ni ya wapiganaji kwa lengo la kuikomboa Tanganyika

Hizi ndio zilikuwa intros za wiki hii nzima mpaka kufikia leo Jumamosi hii alfajiri

Je yajayo yanafurahisha? Ama nayo yataishia njiani

1. Kama kweli Kapteni Tesha yuko hai tafasiri yake ni kwamba ana mawasiliano ya moja kwa moja na kanali Augustine Polepole

2. Kali/taarifa ya mkuu wa majeshi iliyochelewa kukanushwa! Kwanini ilichukua muda sana?

3. Raia aliyetekwa Arusha na kauli ya mkuu wa majeshi. Je ukimya utaendelea ama ni wakati wa vitendo?

4. Ya Mwafwere yatakanushwa ama yatathibitishwa!? Na nani? Athari zake zitakuwaje!!?

5.Ultimatums za Kanali Augustine Polepole je zitakuwa na matokeo ama atapotea tena na kuibuka na nyingine?
6. Habari za TFF na TMF zitazidi kubamba au ndio season imeisha?

Mwisho. Kama kweli Polepole, Mdude na wengine wote bado wako hai (jambo jema sana hili) lakini hili ni kosa kubwa sana kukaa na mateka muda mrefu.. Maana atayajua mengi sana!
Wiki jayo ina mengi yakutuambia

Zaidi soma: Ilivyo ngumu kumlinda mateka! | JamiiForums Ilivyo ngumu kumlinda mateka!
 
Kwa taarifa za ndani ni kwamba captain Tesha alishafukuzwa jeshi na pamoja na wenzake watatu siku nyingi kwa utovu wa nidhamu kabla ya M029 ndo maana akaja na ile press kwa hasira.

Huenda Tesha hana madhara yoyote
 
Hii inaweza kuwa wiki ya kipekee kwa minong'ono mingi na ya kila aina huku "zile habari za chini ya zulia zikiwa nyingi"
Mengi yaliyotokea wiki Hi yana hisia mchanganyiko, uzushi halisi na maigizo..
1. Minong'ono kwamba kapteni Tesha yuko hai salama na huru nje ya nchi akiendeleza harakati

2. Habari za kuibuka kwa mkuu wa majeshi na kutoa onyo kwamba UTEKAJI SASA BASI LA SIVYO....! (Nimeona hii kama imekanushwa jana huko mitandaoni)

3. Kutekwa na kuuawa kwa mkazi mmoja wa Arusha mwenye sintohamu nyingi.. Utekaji huu ni kama vile ulikuwa jibu kwa mkuu wa majeshi aliyesema UTEKAJI sasa basi!

4. Kusambaa kwa habari kwamba mwafwere yamemkuta ya kumkuta

5. Kuibuka kwa kanali Augustine Polepole na kuendelea kutoa ultimatum mdogo wake aachiwe huru haraka pamoja na watu we engine akimtaja na Mdude pia
Kanali naye kampa Pole Mwafwere

6. Habari nyingi za TFF NA TMF.. makundi yanayosemekana ni ya wapiganaji kwa lengo la kuikomboa Tanganyika

Hizi ndio zilikuwa intros za wiki hii nzima mpaka kufikia leo Jumamosi hii alfajiri

Je yajayo yanafurahisha? Ama nayo yataishia njiani

1. Kama kweli Kapteni Tesha yuko hai tafasiri yake ni kwamba ana mawasiliano ya moja kwa moja na kanali Augustine Polepole

2. Kali/taarifa ya mkuu wa majeshi iliyochelewa kukanushwa! Kwanini ilichukua muda sana?

3. Raia aliyetekwa Arusha na kauli ya mkuu wa majeshi. Je ukimya utaendelea ama ni wakati wa vitendo?

4. Ya Mwafwere yatakanushwa ama yatathibitishwa!? Na nani? Athari zake zitakuwaje!!?

5.Ultimatums za Kanali Augustine Polepole je zitakuwa na matokeo ama atapotea tena na kuibuka na nyingine?
6. Habari za TFF na TMF zitazidi kubamba au ndio season imeisha?

Mwisho. Kama kweli Polepole, Mdude na wengine wote bado wako hai (jambo jema sana hili) lakini hili ni kosa kubwa sana kukaa na mateka muda mrefu.. Maana atayajua mengi sana!
Wiki jayo ina mengi yakutuambia

Zaidi soma: Ilivyo ngumu kumlinda mateka! | JamiiForums Ilivyo ngumu kumlinda mateka!

Andiko zuri sana chokozi, Mshana Jr , Sanaa nzuri katika uandishi, be blessed Mpwa!
 
Back
Top Bottom