Wanathamini sana saikolojia, tunakwama wapi?

Wanathamini sana saikolojia, tunakwama wapi?

KENGE 01

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
1,770
Reaction score
4,394
Ni Kenge tena,

Uko duniani(Mataifa yalioendelea) wanazingatia sana wanasaikolojia. unakuta hata muokota uchafu mwisho wa mwezi anafanya appoitment kuonana na Mwanasaikolojia

Baadhi ya Kazi ni lazima uwe na mwanasaikolojia
MFANO;

Bondia na Mke wa bondia
Kwa mujibu wa sheria zao ni lazima Bondia aonane na mwanasaikolojia na Mke wa bondia aonane na mwanasaikolojia ili kushauriwa namna ya kuishi maisha ya ndoa na bondia

Walimu/Wakufunzi
Ni muhimu sana walimu kuonana na wanasaikolojia kwasababu Mwalimu anaweza kuvurugwa uko na Mkewe/mumewe hasira zote zikaishia kwa wanafunzi yaani atawadunda kama ngoma.

Wake wa Wanajeshi
Ili pia ni kundi ambalo ni lazima waonane na mwanasaikolojia kushauriwa kwa ujumla mambo mbalimbali

Wanamichezo(hasa Soka, Rugby, kikapa)
Mfano pale Man united wanautaratibu wa kupeleka wachezaji kwa mwanasaikolojia tena unakaa wiki zaidi ya moja huko,Sancho alipelekwa,Antony alipelekwa alivyorudi akawafunga barca na Martial ndo katoka juzi kati na team nyingine zinautaratibu huohuo ukizingatia wachezaji wanakutana na mengi matusi,Kejeli za mashabiki ila huku bongo sidhani kama team zetu zinautaratibu huo zaidi ya kuamini ULOZI na BIMA ya Afya(HIRIZI)

Sasa nakuuliza mwanabodi Ushawahi kufikiria hata siku moja kuonana na Mwanasaikolojia kupata counselling kidogo maana kwasisi wengine hatujui hata jinsi ya kuwapata hao wanasaikolojia wenyewe!!

Je!Hii inaweza kuwa sababu ya kuwa na idadi kubwa ya matukio yakutisha kama kuchinjana,Kubaka n.k??

Ni zipi faida za kuonana na mwanasaikolojia?

Wako mtiifu Kenge
Nawasilisha
 
Wanathamini Saikolojia kwa sababu, Kila kitu kinaanzia kichwani.

Nakumbuka wakati niko chuo mwaka wa mwisho nliisoma Psychology in Human Behaviour kama somo la ziada, aiseee imenisaidia sana kuishi na watu na kufanya majukumu yangu ya kazi vizuri (nature ya kazi yangu nakutana na watu wengi wenye tabia tofauti)..

Na sisi kama taifa tunapaswa kuchukulia suala la Saikolojia kama kipaumbele, sababu hii nchi watu wengi wana matatiko ya afya akili bila kujua..

Sent from my CPH2363 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: _ly

Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom