Wanataka kunirusha kiwanja nilichonunua. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanataka kunirusha kiwanja nilichonunua.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by manuu, Jul 22, 2010.

 1. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Jamani naomba muongozo juu ya sheria ya umiliki wa kiwanja inasemaje?
  Kuna kiwanja nimenunua Arusha alieniuzia ni mtoto wa mwisho katika hiyo familia ambaye baba mzazi wao alishafariki na kumwachia mke wake kuwa ndio msimamizi wa miradhi sasa na mama aliwagawia watoto wake kila mmoja eneo lake ambapo huyu kijana wa mwisho ndio alieniuzia mimi kwa sababu alikuwa anasoma mzumbe university so akakwama maswala flan ikamlazimu kuuza eneo lake ili aweze kuendelea na masomo basi mi nikanunua hilo eneo ilikuwa ni mwaka 2007 na taratibu nilizofuata nilimshirikisha baloz wa shina,mwenyekiti wa kitongoj na kaka mmoja wa muuzaj nami nikiwa na mashaidi wa upande wangu tukaenda kuandikishiana kwa mwanasheria wa serikal tukamaliza so mi nikapiga fency kile kiwanja nikatulia sasa juz i mean july 2010 amekuja kaka wa yule muuzaji ambaye wameshare baba kumbe yule mzee alikuwa na wake 2 na kila mke alipewa mali zake huyu alieniuzia mimi ni mtoto wa mke mdogo sasa amejitokeza mtoto wa mama mkubwa ambaye naye ameshauza viwanja alivyopewa na amekwenda kunishtaki ofisi ya kijiji akidai kwamba wadogo zake waliuza viwanja vya baba yao bila kumshirikisha yeye so yeye sasa anataka kurudisha pesa za watu walionunua viwanja hivyo ila mi sitaki kurudishiwa hiyo pesa coz hiyo sehemu nilionunua kiwanja ni nzuri kwa shughul yeyote na ni mjin kabisa.Nimepokea barua ya wito toka ofisi ya kijiji ikinitaka nifike hapo ofisin jtano ijayo nikaona bila ya hiyo jtano ngoja niombe ushauri hapa jamvini ili niweze kupata point za kuanzia siku ya kesi hiyo.Ila alieniuzia hilo eneo bado yupo na yupo upande wangu lakini nae anasema ukoo unaweza kumshawishi aseme labda aliuza bila kushirikisha ndugu zake hivyo wanaomba walionunua warudishiwe pesa zao.Ni hayo tu naomba ushauri na sheria kwani inasemaje?
   
 2. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,043
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Wahi ktk mahakama iliyompa yule mama usimamizi wa mirathi chukua copy ya muhtasari wa mgao ama kitu kama hicho, mimi si mwanasheria halafu tulia kama msimamizi alimgawia yule dogo pale basi umewini. Alternatively Dogo aonyeshwe alipewa wapi?
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama procedure uliyoyaeleza ni ya kweli. Hicho kiwanja ni cha kwako. Kama muuzaji aligaiwa kama urithi and at the time of sale ni hakuwa "minor", yaani below 18 years, tukianzia na law of contract ni kwamba document mliyosaini ni kielelezo tosha cha muuzaji kuwa na uwezo wa kuingia katika mkataba wa kukuuzia kiwanja kwa bei mliyokubaliana "fair price". From the moment ulipomkabidhi pesa na wewe kukukabidhi title deed ni kwamba mmeshamaliza mkataba.

  Contract ingekuwa ni void ab initio kama muuzaji angekuwa ni minor, au angekuwa si mmiliki halali wa mali hiyo. Huyo kaka yao anayetaka kukurudishia hela uliyotoa mwaka 2007 ni mpuuzi. Kama mtakubaliana ni lazima ajue kuwa a shilling today is not a shilling tommorow (time value of money) na kwa kuwa wewe ni mwenye mali una haki ya kumtajia hela yoyote unayotaka kuuzia kiwanja chako kama utakuwa willing kuuza hata mara 100 ya bei uliyonunulia.

  Hapo hakuna jipya na ukienda huko kwenye kikao cha usuluhishi waambie kuwa, huhitaji usuluhishi katika mali yako kama wanaona wameonewa waende mahakamani na nina kuhakikishia kuwa utashinda kwa kishindo. Suala lilipo hapo si nani atasema nini bali ni documents zinasema nini. kwa kujiandaa zaidi pitia sheria hizi kwanza
  1. Law of contract ordinance, section ya who can enter into contract

  2. Law of sale of goods, concentrate on when the goods are deemed to be sold

  unaweza pitia na sheria ya ardhi lakini kwa hapa application yake si kubwa sana kwani ardhi is an asset na ndiyo maana hata bank unaweza kuiweka kama dhamana ya mkopo. wasikutishe hao mkuu, mchezo uliisha long time.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mkuu Hofstede, nadhani kiwanja hakina hati hicho (naeza kurekebishwa).
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Manuu... taarifa yako haijitoshelezi; there are more questions than answers
   
 6. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Thanx Bro umenipa mwangaza sana.
   
 7. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Thanx Bro umenipa mwangaza sana.
   
 8. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Mkuu nashukuru ngoja nipitie vifungu hivyo vya sheria nipate mwanga tena.
   
 9. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  You are right Abdul c unajua viwanja vyetu coz mi ninamkataba uliotengenezwa na mwanasheria wa serikali.
   
 10. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  DE NOVO ingekuwa vizuri ungebainisha hata maswal machache ili nitapokujibu nitakuwa nimejifunza kitu kupitia hapo.Thanx.
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya Waarusha wanatabia hiyo .Wanakuuzia then wanarudi kinyume nyume kukuibia au anatafuta mteja wanakubaliana bei ya juu halafu anakumbia anakurudishia hela zako ulilzolipa zamani.Ni upuuzi mtupu. . Hii sio kesi ya kwanza ziko nyingi tu wala usihofu. Mahakamani kesi za aina hii ziko nyingi tu na wanashindwaga kila siku na faini kibao lakini hawasikii.

  1. Nenda na karatasi zako mlizosaini kama ulivyoeleza.
  2. Mwullize alikuwa wapi toka wakati huo
  3.Maana ya kusiani kwa viongozi wa kitongoji ni kudhihirisha kuwa mwuuzaji ndio owner na anafahamika na hao viongozi
  4. Hiyo sell ilkamilka 2007 kama hajaridhika aende mahakamani.
   
Loading...