Wanasiasa wa aina hii wanazidi kutoweka, Je ni faida au hasara kwa nchi?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Mtikila sio jina geni kwa wale walio anza kufuatilia siasa za nchi hii tokea wakati wa awamu ya kwanza.

Ni mwanasiasa aliyekumbana na misukosuko mingi ya kesi na hata kifungo gerezani kwa misimamo yake tena ya kupigania na kuwasemea wasio na sauti ya kujisemea.

Siku za karibuni mwaka 2015 alifariki kwa ajali ya gari yenye utata. Jee wanasiasa machachari na wasio woga kupotea kwao ni faida au hasara? Kwa nani na kwa nini?

Hebu tumsikilize hapa akihutubia huko Zanzibar kuhusu "UNYANI" kama alivyouita mwenyewe.

 
Mzee wa 'Kanakwamba' na 'Haiyumkiniki' maneno aliyopenda sana kuyatumia kwenye hotuba zake

Kasoro yake kubwa ilikuwa chuki yake ya Waziwazi kwa asiokubaliana nao mawazo iwe ya kisiasa, dini, rangi au ki maeneo

1993 alichochea Chuki kali sana dhidi ya Watanzania wenye asili ya Asia akiwaita Magabacholi akiwataka vijana wakapore mali zao

Aliposikia tangazo la Kifo cha Baba wa Taifa Alhamis ya 14 October, 1999 aligawa soda bure pale Kariakoo akisema Nyapara la Waingereza limetoweka

Alipokufa ghafla Horace Kolimba akazusha hadharan kuwa Hayati Mzee Mkapa amemuua Kolimba, akafikishwa Mahakaman akakshindwa kuthibitisha akala Mvua ya Mwaka mmoja

2009 kwny Mkutano wa Umoja wa Makanisa alisambasa Waraka alioupa jina la 'Ugaid wa Jakaya Kikwete' ukapokelewa kwa bashasha na baadhi ya Mababa Askofu

1988 alileta Waraka kwny Mkutano Mkuu wa Ccm akimtuhumu Maskini ya Mungu Mzee Mwinyi eti anataka kuufuta Ukristo Tanzania


Kwny kifo cha Aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Chacha Wangwe akaja na tuhuma kama kawaida yake kumtaja Hadharan Freeman Mbowe kuwa Kamuua Chacha Wangwe


Kwa kifupi alikuwa Mwanasiasa Jasiri lakin Muongo muongo na Mzushi sana
 
Niliskia mahali alipotezwa na maafisa usalama wa nchi jirani baada ya kuanza kuifuatilia hiyo nchi kwenye mambo yake iliyokuwa inayafanya ndani ya mipaka yetu.
 
Nakubaliana na wewe kwamba he was a controversial politician....
Kaz ya wanasiasa ni kusema uongo na ukweli pamoja.... ndio siasa zenyewe..
RIP Rev Mtikila... mwanasiasa mwenye mchango mkubwa sana kwenye uandishi wa sheria za Tanzania
 
Alishinda kuwa kikwete ni gaidi.so he was right. Jamaa hakuwa mwongo alikuwa jasiri na msema ukweli.
 
Back
Top Bottom