Wanasiasa na siasa zimetawala magazeti tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa na siasa zimetawala magazeti tz

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jethro, Nov 11, 2009.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF:

  Kaaa chonjo kipindi kinachorushwa na radio mmoja maarufu hapa nchini hapo jana alfajiri walikuja na Topic Moja kuanzia week ijayo hawato soma tena Magazeti yoyote yenye habari yoyote itakayo husiana na:

  1: Siasa (habari yoyote ihusianayo na siasa ya aina yoyote)
  2: Wanasiasa (habari zozote zihusianazo na wanasias na siasa zao)

  Kwa nini, takribani zaidi ya miezi zaidi ya mitatu hivi na sio miezi tu ni miaka sasa porojo za wanasiasa na siasa zimetawala sana magazeti yetu ya Tanzania.

  Ukichunguza kwa makini ni lini hayo magazeti yametuandikia habari za maendeleo waliyo pata au wafikia wananchi? Zaidi ya ile ya Kilimo Kwanza ambayo hiyo kwa asilimia kubwa ni theory tu, na watanzania wanatakiwa waelimishwe sana juu ya hilo.

  Je wahariri wetu hawa pamoja na kuisomea vyema iyo taaruma yao je ni hiki kweli wanatakiwa kukifikisha kwa wananchi au wanajinufaisha wao kwa kujenga hojazao ili kuuza magazeti na kuwapotezea muda wa kusoma magazeti watanzania???

  Sina mengi zaidi: Ila naunga mkoja kwa mtoa hoja Radio - Clouds FM

  Mwageni hoja zenu bhandugu

   
Loading...