Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,527
- 830,085
Miaka ile ya 2000 wakati wa Gen P. Musharaf wa Pakistan, vyama vingine vyote vya siasa vikiwa vimebanwa mbavu na kuminywa hasa.... Likatokea jambo la nadra sana, sikumbuki vizuri ilikuwaje lakini nakumbuka wanasheria walichokonolewa wakachokozwa.
Hawakukubali, wakaandaa maandamo ya amani kuelekea Islamabad mji mkuu wa Pakistan, maandamano hayo yalitokea miji mingine mikuu kama Peshawar, Lahore na Karachi.
Nakumbuka wiki ya maandalizi ya yale maandamano wanasheria walitishwa sana... Lakini wakashikilia msimamo wao wa kuandamana kwa amani.... Na hatimaye wakaandamana..
Huku kwetu kuna kila dalili ya yale ya Pakistan kujirudia.... Ni wazi na sio siri vyama vya siasa vile vyenye nguvu vimebanwa kila kona na vinafanyiwa hujuma zisizoisha kila uchao, viongozi wanakatishwa tamaa kwa malundo ya kesi, hujuma ni nyingi mno na kesi pia ni nyingi.... Ni mkakati maalum uliosukwa kwa ufundi kudhoofisha na hatimaye kuua kabisa vyama makini vya upinzani..
Lakini siku zote penye nia pana njia! Wote tunajua hofu waliyokuwa nayo watawala kwa Lisu kuchaguliwa kuwa rais wa chama cha wanasheria Tanganyika! Tulishuhudia vibweka vya kila aina.... Wanasheria wakagoma kuburuzwa, wakagoma kupangiwa wakagoma kupelekeshwa! Na kubwa kuliko yote wakagoma KUNUNULIWA..
Mshikamano wao wakati ule wa uchaguzi likikuwa jambo geni, wengi walidhani baada ya pale wataachana njiapanda.... HAWAKUFANYA HIVYO..... kauli yao imekuwa SOLIDARITY FOREVER!
Mambo ya nadra yameendelea kutokea kwenye kaliba hii ya wasomi wanataaluma mahiri.... Tumeshuhudia kwenye kesi ya Lisu, tumeshuhudia kwenye kesi ya mwanamama machachari Bi Fatma Karume.... kuna bonding ya aina yake kwa hii kaliba ya sheria... Mamlaka hazipedi kabisa hili jambo lakini pengine ndio ule wakati umetimia sasa.....
A long way to freedom!
Sent using Jamii Forums mobile app