Wanasheria tupeni ufafanuzi kuhusu suala hili la matokeo ya uchaguzi

mendz

Senior Member
Dec 9, 2013
144
49
Kwa nini UKAWA wasiende mahakamani kudai haki yao ya kuhakikisha ibara ya 41 kipengele cha 6 kimetimizwa?

Kipengele hicho kinasema kuwa Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote.

Kama UKAWA wana ushahidi kwamba Lowassa ndie aliyepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote, kwa nini wasiende mahakamani kutaka kipengele hicho hapo juu kitimizwe?

Kipengele cha 7 kinasema iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hiyo ya 41 basi hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguzwa kuchaguliwa kwake.

Kwa mtazamo wangu, kipengele cha 6 kwanza inabidi kitimizwe ili kipengele cha 7 kiweze kuwa na nguvu za kisheria.

Wanasheria mnasemaje?
 

Attachments

  • 12195903_167240800289932_6719626614609105795_n.jpg
    12195903_167240800289932_6719626614609105795_n.jpg
    19.7 KB · Views: 101
Watu vichwa vinawauma.

Tuna wanasheria makini kabisa ambao wanatakiwa wasimamie hoja ya compliance ya Ibara number 41. Wanahitaji kusimamia ibara hiyo kutengua utangazwaji wa Magufuli kwa sababu kifungu cha 6 kimekiukwa!. Na hivyo kwa misingi hiyo, uteuzi wa magufuli siyo halali.
 
Back
Top Bottom