mzalendokweli
JF-Expert Member
- Apr 21, 2012
- 579
- 137
Usizungumzie swala hilo kwan liko mahakaman.
Tatizo kubwa la Watanzania wengi MMM, ni wasahaulifu na hawana maamuzi!!
ha ha ha ha ha Mkuu SJumaa26, ukifika kwenye ofisi yangu ndio ungetambua anyway sikoupande wowote wa kimaamuz ya public.Na wewe pia unalalamika, so no difference! Hata hivyo hapo kwenye bold ulipaswa kuandika hatu na sio hawa-. Unategemea nani achukue hatua wakati wewe unaishia ku-post tu JF? Huu nao ni UDHAIFU wa Watz!
If you remain neutral in cases of injustice, that means you have chosen the side of the oppressor. You are either with us or against us! Period.ha ha ha ha ha Mkuu SJumaa26, ukifika kwenye ofisi yangu ndio ungetambua anyway sikoupande wowote wa kimaamuz ya public.
KUna uwezekano kwamba lolote kubwa laweza kuchukuliwa dhidi ya wale wanaodaiwa kuchukua rushwa?
Kwamba Mhando (Mkurugenzi wa Tanesco) amejipa mkataba yeye na mke wake na kukiuka waziwazi sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya 1998 halina shaka. Lakini cha kushangaza ni kuwa ati Waziri anaenda kumlipua Bungeni badala ya aliyemteua kumfukuza kazi, kumtia pingu na kuhakikisha anaingia gerezani yeye na wote waliowezesha dili hilo.
MMM
Katika umaskini wetu tumejifunza kufurahia! MM
Mzee Mwanakijiji,
Hii nchi ina sheria na taratibu zake, huwezi kukurupuka tu kumtia mtu pingu na kumtupa lupango bila kufuata hatua stahili. Kama ndio hiyo Tanzania mnayotaka kutuletea basi itakuwa vurugu mechi mitaani. Tulieni msikie hatua zitakazochukuliwa usikurupuke tu kutaka kuona watu wanatiwa pingu mwishowe yanakuwa yale yale ya Dowans wanasiasa kina Zitto kufurahisha wananchi kama wewe mwishowe ina tu cost nchi nzima tunalipa fidia mabilioni.Msipende kuhadaa wananchi...
Usisahau kwamba huo ujinga tulonao wa kushabikia matukio ndo kete yao ili kutuburuza.Mkuu Mzee Mwanakijiji umeongea na nakubaliana na uchambuzi wako
Ila tatizo watu wetu ni wasahaulifu sana na ni watu wa matukio
Likitokea hili wanasahau lile la mwanzo na kuanza ushabiki wa hili jipya na hakuna hatua zozote wanazochukua kuonyeshwa kukerwa kwao na hilo lililopita
Asante sana kwa uchambuzi wako
Maneno mengiii, ili kutaka jamii ikuone umesema jambo la maana! Ukweli utabaki pale pale wewe subiri siku ukishika nchi uje na hizo SERA zako zinazo wezekana, lakini kwa sasa endelea tu kupiga domo watu wanapiga kazi.
Tulieni mpaka tushibe!! tutaunda tume au tutakamata kichaa tumpeleke mahakamani ili kuziba midomo michafu (usiingilie mahakama). Tufuate taratibu na sheria!! EPA, nani alikamatwa!!?? Richmond nani alikamatwa!? hivi Rostam ni mmiliki wa DOWANS na Richmond yuko wapi? Rostam aliyemfadhili JK kwenda ikulu akamatwe na nani? Sheria zipi na taratibu zifuatwe? Nyie wezi wa EPA rudisheni fedha mlizoiba kidogo kidogo ama tusijelaumiana!! by JK. hizi ndizo taratibu na sheria!!Mzee Mwanakijiji,
Hii nchi ina sheria na taratibu zake, huwezi kukurupuka tu kumtia mtu pingu na kumtupa lupango bila kufuata hatua stahili. Kama ndio hiyo Tanzania mnayotaka kutuletea basi itakuwa vurugu mechi mitaani. Tulieni msikie hatua zitakazochukuliwa usikurupuke tu kutaka kuona watu wanatiwa pingu mwishowe yanakuwa yale yale ya Dowans wanasiasa kina Zitto kufurahisha wananchi kama wewe mwishowe ina tu cost nchi nzima tunalipa fidia mabilioni.
Msipende kuhadaa wananchi...
Usiwalaumu wananchi Mkuu. Haya mambo yanahasisiwa na Chama Tawala ili yawe hivi, recently kuna kitengo maalumu Ikulu cha kuasisi upuuzi huu, ili tu Mfalme asizungumziwe. Na wamefanikiwa.Mkuu Mzee Mwanakijiji umeongea na nakubaliana na uchambuzi wako
Ila tatizo watu wetu ni wasahaulifu sana na ni watu wa matukio
Likitokea hili wanasahau lile la mwanzo na kuanza ushabiki wa hili jipya na hakuna hatua zozote wanazochukua kuonyeshwa kukerwa kwao na hilo lililopita
Asante sana kwa uchambuzi wako
Usisahau kwamba huo ujinga tulonao wa kushabikia matukio ndo kete yao ili kutuburuza.
Na kwakuwa walisha litambua hilo, ndio maana mazingaombwe hayeshi, kila siku kuna ingizo jipya!
Ukihoji lililopita limeishia wapi, utasikia aaa bwana mdogo kitu iko kwa mahakama usiijadili/ulizia.
mwisho wa siku uchaguzi huo tunawapa tena nafasi kwa kete hizo hizo za kujinasibu kwamba tunawajali na tunapambana kweli kweli na wezi,kama mnavyoshuhudia kesi ziko mahakamani.
Mkuu Sangarara nakubaliana na wewe kabisaUsiwalaumu wananchi Mkuu. Haya mambo yanahasisiwa na Chama Tawala ili yawe hivi, recently kuna kitengo maalumu Ikulu cha kuasisi upuuzi huu, ili tu Mfalme asizungumziwe. Na wamefanikiwa.
Tulieni mpaka tushibe!! tutaunda tume au tutakamata kichaa tumpeleke mahakamani ili kuziba midomo michafu (usiingilie mahakama). Tufuate taratibu na sheria!! EPA, nani alikamatwa!!?? Richmond nani alikamatwa!? hivi Rostam ni mmiliki wa DOWANS na Richmond yuko wapi? Rostam aliyemfadhili JK kwenda ikulu akamatwe na nani? Sheria zipi na taratibu zifuatwe? Nyie wezi wa EPA rudisheni fedha mlizoiba kidogo kidogo ama tusijelaumiana!! by JK. hizi ndizo taratibu na sheria!!
Nafikiri mkuu Kisoda2 haya mambo ya kusema kesi iko mahakamani haifai kuhojiwa yafikie mwisho wake tuone kile kinachotokana na hizo kesi mahakamani
Maana inawezekana kesi mahakamani then mshatakiwa anakuja kuachiliwa kwa kukosa ushahidi au kutokuwa na kesi ya kujibu na hapo moto wa ile kitu unakuwa umeisha kabisa
Tufikie mahali tuhoji haya mambo tuone wahusika wanapelekwa kweli mahakamani na kesi yao inaamuliwa kwa kipindi kifupi na tunaona uwajibikaji au wa kurudisha kile kilichopotea au kufilisiwa
Kesi za akina Mramba na Yona mpaka leo ni danadana hatuoni maemdeleo na itafika 2015 tutadanganywa kuwa tumewafikishamafisadi mahakamani na si mnaona akina fulani na kura tutawapa tena
haya ndio yanayotumpumbaza wananchi tuache kuhoji mambo ya maana tuwasikilize uwongo wanaotulisha
Mkuu Sangarara nakubaliana na wewe kabisa
Kuna sehemu wamekaa watu wanaanzisha zengwe wananchi wajadili kwa hasira na pupa wakiona single yao inaanza kuchuja wanalianzisha tena jingine ili wananchi wasahau lile la kwanza zito waanze kujadili jepesi
yaani hizi single zao hazikao sokoni kabisa yaani zinatolewa mara kw amara wanapoona kuna haja ya kutoa single kuwasahaulisha wananchi na yale yaliyopita
Wasahau mpaka shida zao waanze kujadili lile tukio
Mkuu, Ninachokiona ni kwamba, wanajisababishia pressure kubwa dhidi yao uko mbeleni, sababu soon watu wataachana na Keyboards na kwenda kuongea na wananchi uso kwa uso. Na hili inabidi tujiandae nalo sababu uwezu wa wenzetu wengi ni mdogo sana na kwa sababu wengi pia hawana matumaini na maendeleo ya ziada wanakuwa wepesi sana kusahau wanachokitaka ni nini wanaishia kununua hizi stupid singles.