Mc cane
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 5,570
- 10,506
- Thread starter
- #41
Kwahiyo ukiacha kufanya mapenzi kuna nini cha ziada katika ndoa?Uwapo kwenye ndoa,tendo la ngono baina ya Mme na mke linageuka kuwa tendo takatifu. Tendo la ndoa limebeba ndoa kwa kiasi kikubwa kwa sababu moja ya wajibu Mkubwa na agizo kuu walilopewa wanandoa na Mungu ni kuzaa watoto na kuwalea vema. Kwa hiyo tendo la ndoa siyo kila kitu kwenye ndoa Bali ni sehemu tu ya ndoa. Kuna matendo mengine makuu pia na yakikosekana hayo basi pamoja na matendo ya ngono ni kazi bure mf. Kupendana, Kusameheana na Kuvumiliana. Kwenye kuvumiliana hapo ina maana kuna wakati mmoja Wa wanandoa anaweza kuwa hana uwezo Wa kuzalisha au kuzaa japo anafanya tendo la ndoa na mwenzake bado mtatakiwa kukubali hali hiyo pasipo kinyongo. Haya ni machache tu ndoa ni zaidi ya tendo la ndoa.