Wanasema Ndoa ni Zaidi Kufanya Mapenzi, Naomba 'Components' Nyingine za Ndoa

kukosea KUJENGA NYUMBA utaibomoa KULIKO KUKOSEA KUOA,,,na UPAPASWA uelewe kwamba NDOA NI ZAIDI YA TENDO LA NDOA,,ingawa lile TENDO NDY LINAKAMILISHA NDOA,,,Nina maana kwamba kila BINADAMU ANAKUWA NA NYOTA YAKE,,,,ktk MAISHA,,,, unapooa MWANAMKE ambaye ana NIKSI NA MIKOSI basi elewa UTAPATA HASARA KTK MAISHA NA MAMBO YAKO,,,na ukioa MWANAMKE ambaye ana nyota nzr basi ni chanzo cha KUFUNGUKA MAMBO NA MAISHA YAKO,,,Nina maana kwamba ktk maisha ya NDOA unaweza ukawa unatumia NYOTA YA MKEO BILA KUJIJUWA,,,ndy maana unakuta MTU akiwa na UGOMVI WA MARA KWA MARA NA MKE,,,mambo huvurugika,,,,na kujiona UMEROGWA,,,tuwapende wake ZETU,,, tuwasikilize mawazo yao,,HUENDA HAPA TULIPO NDY WAO WALIOTUPANDISHA AU KUTUSHUSHA..,,,,huo ni USHUHUDA 100%
Upo sahihi mkuu kiujumla mm nimekuelewa sn na atakae pinga hili jua hayupo kwenye ndoa
 
me ntaoa kwa sababu nataka penzi kutoka kwa huyo binti, na sio kingine.
 
Ndoa inaweza kuvunjwa huko kanisani ikiwa mmoja anaefunga ndoa Hawezi kufanya tendo La ndoa.
Hii ina maana ndoa natendo lake Ndio msingi wa ndoa.
Mengine yote unaweza kufanya na yeyote Mfano unaweza kushauriwa, kupikiwa, kupewa fedha n. K Na yeyote lakini ole wako ufanye tendo La ndoa na mwingine asie mwenzi wako hiyo inakua Kesi kubwa na chanzo cha matatizo.
Ndoa bila tendo la ndoa Sio ndoa ni urafiki Wa karibu tu Kama urafiki mwingine.
 
Ujue unaweza kupata sex bila hata kuoa na kuolewa.
Watu wanatakiwa walitambue Hilo hasa wanawake.
Wanawake wamejigeuza siku hizi kuwa kazi yao ndani ya ndoa Ni kutoa tundu tu.
Kazi zingine zote wanaachia house girl.
Ndoa ni zaidi ya kufanya ngono
Kuna mapenzi mengine mnayajenga mnapokuwa pamoja na kufanya Mambo mengine.
Mwanaume anachukuliwa Kama kichwa Cha familia.
Ndio visionary leader, mlinzi(social na economical security). Anatakiwa kumuonesha upendo mke na familia.
Mwanamke anapaswa kuhakikisha familia inakula chakula Safi, familia iko salama kiafya, kisaikolojia nk.
Mkigeuza ndoa sehemu ya sex mtakuwa na watoto wasioeleweka.
Kama mtu anadhani kuolewa Ni kwenda kuoffer sex ni Bora awe muuzaji tu mtaani. Asiende kumtia stress kijana wa watu akaanza kumkufuru Mungu.
 
Ndoa inaweza kuvunjwa huko kanisani ikiwa mmoja anaefunga ndoa Hawezi kufanya tendo La ndoa.
Hii ina maana ndoa natendo lake Ndio msingi wa ndoa.
Mengine yote unaweza kufanya na yeyote Mfano unaweza kushauriwa, kupikiwa, kupewa fedha n. K Na yeyote lakini ole wako ufanye tendo La ndoa na mwingine asie mwenzi wako hiyo inakua Kesi kubwa na chanzo cha matatizo.
Ndoa bila tendo la ndoa Sio ndoa ni urafiki Wa karibu tu Kama urafiki mwingine.
Hata ngono ambalo linaitwa tendo la ndoa unaweza kulipata kwa mtu mwingine bila kuoa au kuolewa.
Na ilikuwepo na haiji kuisha.

Biashara ya ukahaba Ni moja ya the oldest business duniani.
Hata kwenye agano la kale ipo!
Walikuwa wanamuuzia Nani?
 
Its true, but not all of them.
Nimeendeleza quote yako iliishia njiani "ni maneno maarufu ya Trevor Noah
Let me attach (see below pic)
img_2520.jpeg
 
Wasalam

Katika maisha yangu nimekuwa nikisikia mara kwa mara kuwa Ndoa ni zaidi ya kuwa na uhakika wa kucheza kibaba baba na kimama mama usiku (au muda wowote fursa ikipatikana).

Ki ukweli kwa kipindi kirefu huo ndio umekuwa uelewa wangu.

Naomba mnifumbue macho, je kwenye Taasisi ya Ndoa kuna mambo gani mengine ambayo Wanandoa wanaweza kuyapata?

Nawasilisha
Mkuu; Hebu soma hili halafu utafakari hayo maneno ambayo nimeyabold: ......unampokea........awe Mme/Mke wako tena waahidi kuwa MWAMINIFU kwake katika TAABU na RAHA katika MAGONJWA na AFYA, UMPENDE na KUMHESHIMU SIKU ZOTE za MAISHA yako?
Kwa hiyo Ndoa si Lelemama. Ingekuwa ni hicho ulichosema umekiamini kwa siku nyingi mbona hilo linafanyikaga hata kabla ya Ndoa?
 
Dah...mnawachanganya madogo...tendo la ndoa... kwa kizungu ni sex...unaweza kulipata hata bila ndoa...msiwaingize madogo kwenye mikataba ya kilaghai..
 
Ndoa inaweza kuvunjwa huko kanisani ikiwa mmoja anaefunga ndoa Hawezi kufanya tendo La ndoa.
Hii ina maana ndoa natendo lake Ndio msingi wa ndoa.
Mengine yote unaweza kufanya na yeyote Mfano unaweza kushauriwa, kupikiwa, kupewa fedha n. K Na yeyote lakini ole wako ufanye tendo La ndoa na mwingine asie mwenzi wako hiyo inakua Kesi kubwa na chanzo cha matatizo.
Ndoa bila tendo la ndoa Sio ndoa ni urafiki Wa karibu tu Kama urafiki mwingine.
Mkuu, naomba nitofautiane na ww kidogo hapo kwenye kuvunjika kwa ndoa na sababu ikiwa ni mmoja wenu hawezi kufanya tendo la ndoa. Hoja inakuja kwamba kwa mfano katika pilikapilika za maisha yenu ikatokea kwamba mmoja wenu anapata ajali au ugonjwa na ugonjwa huo ukamwathiri kiasi kwamba hataweza tena kufanya tendo la ndoa. Hapo utatakiwa kuendelea katika ndoa hiyo na ndoa haitavunjwa.
Lakini pia inawezekana Ndoa ikavunjwa kutokana na Hatari ya kudhuru Uhai kati yenu. Kwa mfano jaribio la kuua (Kwa sumu au njia nyingine) linalojirudia-rudia au vitisho, kipigo kilichokithiri, Uasherati/Uzinzi n.k. Kwa kifupi ni kwamba zipo sababu nyingine pia ambazo ndoa inaweza kuvunjwa sio tu kwa kushindwa tendo la ndoa.
 
Kinachofanya ndoa ionekane ni kufanya mapenzi ni pamoja na lile tendo lenyewe linaitwa tendo la ndoa.

Inamaana hilo tendo ndio limebeba ndoa?
Uwapo kwenye ndoa,tendo la ngono baina ya Mme na mke linageuka kuwa tendo takatifu. Tendo la ndoa limebeba ndoa kwa kiasi kikubwa kwa sababu moja ya wajibu Mkubwa na agizo kuu walilopewa wanandoa na Mungu ni kuzaa watoto na kuwalea vema. Kwa hiyo tendo la ndoa siyo kila kitu kwenye ndoa Bali ni sehemu tu ya ndoa. Kuna matendo mengine makuu pia na yakikosekana hayo basi pamoja na matendo ya ngono ni kazi bure mf. Kupendana, Kusameheana na Kuvumiliana. Kwenye kuvumiliana hapo ina maana kuna wakati mmoja Wa wanandoa anaweza kuwa hana uwezo Wa kuzalisha au kuzaa japo anafanya tendo la ndoa na mwenzake bado mtatakiwa kukubali hali hiyo pasipo kinyongo. Haya ni machache tu ndoa ni zaidi ya tendo la ndoa.
 
Back
Top Bottom