Wanasayansi watengeneza mbegu za kiume.

Wanasayansi watengeneza mbegu za kiume.

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,324
Reaction score
2,494
Wanasayansi watengeneza mbegu za kiume. ''Seli za mbegu za kiume zimetengenezwa katika maabara kwa mara ya kwanza na hivyobasi kuwapa matumaini wanaume wasio na uwezo wa kupata watoto. Kampuni moja nchini Ufaransa imedai kwamba imefanikiwa kubadilisha vipande tofauti vya maumbile hadi kupata mbegu za kiume zinazoweza kutoa mtoto kwa mara ya kwanza.

Iwapo uzinduzi huo utathibitishwa, huenda ukabadilisha maisha ya wanaume wengi duniani ambao hawawezi kutoa mbegu za kiume. Maabara ya Kallistem, kituo cha kibinafsi cha utafiti kilichopo mjini Lyon kimesema kuwa kitaweza kufanya majaribio katika kipindi cha miaka miwili. Iwapo uzinduzi huo utaingia sokoni, kampuni hiyo inataraji kuwatibu watu 50,000 kila mwaka soko ambalo linaweza kuwa na thamani ya pauni bilioni 1.7.

Hatahivyo matokeo ya utafiti huo hayajachapishwa ama hata kuthibitishwa huku wataalam wa Uingereza wakichukulia uvumbuzi huo kama uvumi tu. Kalliste imesema kuwa imefanikiwa kubadilisha seli za kawaida katika mbegu za kiume hadi mbegu za kiume zilizokomaa.'' Je habari hii italeta heshima kwenye ndoa kwa wanaume wasiokuwa na uwezo? Ila ni shughuli mwanaume unagonga we empty. Ni uamuzi mgumu kumwambia mkeo katafute mtoto popote nitamlea.

Source: Ufyetele blogspot.com
 
Tanzania zinaanza kupatikana lini niwahi foleni?
 
Mbegu ya kiume ndio uhai. Kama haikuyika kwa mwanaume haitaumba binadamu
 
Khaa!! Miye sijaelewa vizuri. Yaani wao wanahangaika kutengeneza mbegu hizi wakati huku kwetu zinatupwa tu na ndomu yake kwenye majalala?? Bora wangekuja huku wakaokota za bure kabisa :confused2:
 
Khaa!! Miye sijaelewa vizuri. Yaani wao wanahangaika kutengeneza mbegu hizi wakati huku kwetu zinatupwa tu na ndomu yake kwenye majalala?? Bora wangekuja huku wakaokota za bure kabisa :confused2:

Hata kwenye mabafu ya uswazi mbona zpo za kutosha
 
In the next 20/30 years the world will be made up of programmed & controlled mudhafools.
 
Back
Top Bottom