Wanasaikolojia hebu mnielewe katika hili.

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
995
1,508
Wanasaikolojia wengi kama sio wote wanashauri watu wawesema mahasibu yanayowakumba ili wasaidike wakiamini kwamba watu hawasemi wanakaa na mambo moyoni kitu kinachopelea kufanya maamuzi magumu ili hali wangesema wangesaidika.

Ukweli ni kwamba sio kwamba watu hawawashirikishi watu matatizo yao hapana,kinachowafanya watu wafanye maamuzi magumu ni kupuuzwa na watu watu wao wakaribu na mara nyingi ni ndugu wa damu kabisaaaa.

Mtu unamshirikisha jambo na unaona kabisa na unauhakika kabisa lipo ndani ya uwezo wake ila anachukulia poa anakwambia tu Sorry, God will make a way,ndio imeisha,utafikiri kwamba wakati anashirikishwa mhanga hakujua kwamba God always make a way to escape,hajui kwamba pale ndio anaitafuta hiyo way kupotia yeye,RUBBISH,kibaya zaidi wakiachana ndio imetoka hiyo hata kumpigia simu kujua kama amefanikiwa au lah hapigi Ana mute.

Kuna familia nyungine ukienda kuomba msaada badala yakushughurikia tatizo lotatuliwe wanaanza kulijadili tatizo,kukukosoa mambo lukuki ,yaani wana mu-electrify anaanza kuhisi hapo ndio ukomo na akiondoka hata hawajali.

It's an experience to me and not a story to tell,people are too much stupid.

Kwa upande wangu mimi I live differently, I trust on my self than any,highly emotionally developed,nikiamua kukushirikisha ukaleta stories nakucharua.

Wanaosababisha matatizo ni hawa tunaowashirikisha mambo yetu.
 
Kwa maisha yetu ya kitanzania ni ngumu mtu kuelezea matatizo yake akasaidiwa,wale wenye uelewa kidogo au wapenda kusoma huwa wanapata msaada kidogo ktk vitabu,au wanasaikolojia wa mitandaoni kama YouTube.Ukimuelezea mtu yanayokukabili moyoni jiandae kuumia mara mbili zaidi kwasababu watu wataanza kukupa lawama au na wao kukuelezea shida zao.
 
Kwa maisha yetu ya kitanzania ni ngumu mtu kuelezea matatizo yake akasaidiwa,wale wenye uelewa kidogo au wapenda kusoma huwa wanapata msaada kidogo ktk vitabu,au wanasaikolojia wa mitandaoni kama YouTube.Ukimuelezea mtu yanayokukabili moyoni jiandae kuumia mara mbili zaidi kwasababu watu wataanza kukupa lawama au na wao kukuelezea shida zao.
Kabisaaa yaani
 
Kwenye Maisha changamoto hazikwepeki.

Ukilijua hili kamwe hutosumbuka sana,Ila jitahidi ukienda kuomba ushauri usiende tayari ilihali una majibu yako.

Yaani kama kwa daktari vile usilazimishe majibu Fulani kabla ya vipimo sahihi.

Kumbuka KUJIELEZA ni sehemu ya TIBA,kwani Kuna mtu anahtaji tu wa kumsikiliza au kuwa nae wakati wa magumu anayopitia.

Usidharau jambo katika utatuzi wa matatizo yanayokisumbua kichwa chako,Kwani mrundikano wa vitu vidogo kichwani pasi na kuvisema siku zote ndio upelekea kuwa na makubwa hasa Ambayo uhesabika yenye madhara.
 
Ukiwashirikisha wengi ,ndo unakuwa main topic,wengine hata wanaweza fanya sherehe kufurahia mapito yako,ila mimi nilijifunza kumshirikisha mtu usiemfahamu. Mfano hata dereva tax,mama ntilie,au ukiona wazee hata usiowafahamu.
Kabisa yaani
 
Back
Top Bottom