Mambo ni mengi muda hautoshi. Twende kwenye orodha moja kwa moja bila kupoteza muda.
1. FILBERT BAYI
Mzee wetu kaongelewa kwenye makala mengi mno duniani kiasi kwamba shirikisho la ridha duniani limehifadhi kumbukumbu zake kwenye makumbusho ya shirikisho huko Ufaransa. Mzee Filbert Bayi anakumbukwa kwa kuvunja rekodi ya dunia mwaka 1974 kwenye mbio za 1500 na pia record ya maili moja mwaka 1975. Lakini ana record nyingine ya dunia ya mbio za ndani za 5000m (world indoor 5000m record) ambayo wakati anaivunja shirikisho la dunia lilikuwa halitunzi record zake. Mwaka 1981 jijini Toronto, Canada Filbert Bayi aliweka indoor world record 5000m.
Hadi leo kitaifa hakuna mtanzania aliyevunja rekodi za Mzee Bayi za 1500m, Mile, 3000m na 3000m steeplechase (kuruka viunzi). Kitaifa Mzee Bayi ndo mwenye hizo rekodi alizoziweka zaidi ya miaka 40 iliyopita.
2. SULEIMAN NYAMBUI
Tofauti na wanariadha wengi Mzee Suleiman Nyambui na Filbert Bayi ni wanariadha wasomi waliosomea nchini Marekani. Mzee Nyambui kapata Bachelor na Masters Degrees toka University of Texas at El paso (UTEP). Mzee Nyambui bado anashikilia rekodi za kitaifa za indoor za 3000m na 5000m. Kama ilivyokuwa kwa Bayi, Nyambui pia alishawahi kuvunja world indoor 5000m record February 1981. Pia kwenye mbio za mwaka 1974 wakati Bayi anavunja rekodi ya 1500m, Mzee Nyambui alikuwepo na kukimbia kwa muda wa 3:39. Kilichomgharimu sana Nyambui kutovuma ni kukimbia wakati Bayi akiwa kwenye ubora wake.
3. GABRIEL GEAY
Huyu GenZ ni hatari mno. Anashikilia rekodi za taifa kwenye 15km, 20km, Half Marathon, 25km, 30km na Marathon. Ni miongoni mwa wanariadha wakubwa duniani kwa sasa wanaolipwa pesa nyingi na kupewa mikataba minono na ADIDAS. Tatizo wanariadha sio watu wa show offs ila wangeamua kuwa machachari wangekuwa wanatrend kila kona ya dunia. Hawa viumbe ni mamilionea wakimya.
4. MAXIMILLIAN MATLE
Komredi Maximillian Matle Iranqhe amabye kwa sasa ni meya wa jiji la Arusha kwa tiketi ya CCM hawezi kosa kwenye orodha hii tukufu. Meya Max alikiwasha sana kwenye mbio za 800m na 1500m mwanzoni mwa miaka ya 90.
ITAENDELEA...